maji kuonganishwa kutoka victoria ,old shinyanga ,kishapu,mwadui na kulandoto
maji kuonganishwa kutoka victoria ,old shinyanga ,kishapu,mwadui na kulandoto
Waziri wa maji na
umwagiliaji injinia Gerson Lwenge
ameweka Jiwe la Msingi kwenye mradi wa upanuzi wa mtandao wa Maji ya ziwa
Victoria kutoka old shinyanga hadi kishapu kupitia maganzo,mwadui na kolandoto.
Mara baada ya kuweka
Jiwe la msingi waziri injinia Lwenge amezungumza na hadhara ya wakazi wa mji wa
Mhunze katika wilaya ya kishapu,na kuwahakikishia upatikanaji wa huduma ya maji
ya mradi mkubwa wa ziwa viktoria siku tatu zijazo
Awali akizungumza
katika ofisi ya mkuu wa Wilaya ya kishapu injinia Lwenge amewaagiza viongozi na
watendaji katika halmashauri zote za wilaya ya kishapu kuhakikisha wanakuwa na
mpango madhubuti wa kukabiliana na uhaba wa maji kwa kutunza vyanzo na
miundombinu ya maji
Waziri Lwenge alikuwa
na ziara ya siku moja mkoani Shinyanga lengo ni kuhakikisha wananchi wanapata
huduma ya maji safi na salama,ikiwa na dhamira ya serikali ya awamu ya tano
kufanya kazi kwa maboresho.
….cue in..waziri wananchi
kupata huduma ya maji…
Kwa upande wao wananchi
wa wilaya ya kishapu wameipongeza serikali kutatua kero ya maji iliyowasumbua kwa muda mrefu na
kusema kuwa mradi huo mkubwa wa maji ya ziwa viktoria utakuwa chachu ya
maendeleo katika wilaya yao
Wamesema ni muda mrefu
wananchi wa kishapu wamekuwa wakikabiliwa na ukosefu wa huduma ya maji,hali
ambayo imekuwa ni usumbufu na kikwazo kwa maendeleo yao
Post a Comment