Header Ads

simu za mikononi kufichua siri


Simu za fichua siriImage copyrightTHINKSTOCK
Image captionJe wajua uwezo wa simu yako?
Chembechembe zilizopatikana kwenye simu za mikononi zinaashiria kiwango cha afya na maisha ya mmiliki, ikiwemo matibabu na aina ya chakula anachopendelea.
Mwanasayansi kutoka California amebainisha kuwa kati ya simu arobaini zilizochunguzwa, zimegundulika kuwa na cafeini pamoja na vipodozi vya ngozi,
Utafiki unaonyesha kuwa hata kunawa mikono mara kwa mara hakutazuia kusambaa kwa chembechembe hizo katika vitu vingine.
Watafiti kutoka chuo kikuu cha California kilichopo mjini San Diogo, wamefanya tafiti za sampuli 500 kutoka kwenye simu 40 za watu wazima na mikono yao.
Dkt Amina Bouslimani ambaye ni mwanasayansi msaidizi katika utafiti huo alisema matokeo yalionyesha kuwa,
''Kwa kuchunguza chembechembe zilizoachwa kwenye simu zao,,, tunaweza kusema kwamba kama mtu ni mwanamke, na anatumia vipodozi, na kupaka rangi nywele zake, anakunywa kahawa na, anapendelea bia kuliko wine, anapenda kula vizuri, anatibiwa msongo wa mawazo, anaikinga ngozi na jua, kupulizia marashi,mara nyingi hupenda kutumia muda wake mwingi nje ya nyumba …. na vitu vingine kama hivyo,'' ..alieleza.
Mara nyingi Chembechembe hizo zinaweza kutoka kwenye ngozi na jasho la mikononi kwenda kwenye simu zao.
Dawa za mbu na zile za kuzuia miale ya jua zimekuwa zikidumu kwa muda mrefu kwenye ngozi na kwenye simu hata kama hazijatumiwa kwa kipindi cha mwezi mmoja.
Tafiti zilizopita zilizofanywa na watafiti haohao zinaonyesha kuwa hata kama mtu hajanawa kwa siku tatu hivi, bado ataonekana kuwa msafi na mrembo.
Utafiti umebainisha njia za majaribio kama vile,
· Kuonyesha umiliki wa kifaa bila kutumia alama za vidole.
· Kuangalia kama mtu alikuwa anatumia dawa
· Kutoa taarifa sahihi za mtu husika kama ameshika uchafu,
Mtafiti anataka kujua zaidi juu ya wingi wa bacteria walioko kwenye ngozi zetu na wanaanisha nini kuhusu sisi.
Mwandishi mkongwe prof Pieter Dorrestein amesema kuwa Mwili wa binadamu una bakteria ambao si chini ya 1000 tofauti tofauti katika sehemu mbalimbali za mwili

No comments