Jumla ya wanafunzi 16,907 kati ya 25,413 wa shule za msingi katika mkoa wa Shinyanga wamechaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari
Jumla ya wanafunzi
16,907 kati ya 25,413 wa shule za msingi
katika mkoa wa Shinyanga wamechaguliwa kuendelea na masomo ya sekondari kidato
cha kwanza kwa mwaka 2017,ufaulu ambao ni sawa na asilimia 66.53 ya waliofanya
mtihani,wa kuhitimu darasa la saba mwezi septemba mwaka huu
Akitangaza matokeo ya
uteuzi wa wanafunzi watakaojiunga na
kidato cha kwanza kwa mwaka wa masomo 2017,katibu tawala mkoa wa shinyanga
ALBERTH MSOVELA anesema matokeo na ufaulu huo umetokana na usimamizi,utendaji
na Jitihada baina ya walimu,watendaji na wanafunzi wenyewe.
Amesema matokeo hayo
yametoa fursa kwa mkoa kushika
nafasi ya 15 kati ya mikoa 26 iliyopo hapa nchini huku shule mbili zikiwa
kwenye kumi bora baada ya kushika nafasi ya kwanza na ya pili.
Diwani wa kata ya
kambarage katika manispaa ya Shinyanga Hassan Mwendapole,ni miongoni mwa wajumbe
waliohudhuria kwenye kikao cha kutangaza uteuzi wa wanafunzi, ambaye alitaka
kupata ufafanuzi wa mambo kadhaa ikiwemo mgawanyo wa nafasi za kwenda kusoma
shule za bweni
---
Akijibu hoja ya mheshimiwa
MWENDAPOLE afisa Elimu wa mkoa wa Shinyanga Mohamed Kahundi amesema ushirikiano wa wazazi kufuatilia mwenendo
wa watoto,inahitaji kipaumbele na kwamba suala la kukariri lina taratibu zake
kwa kuwa lipo kisera.
Aidha wadau wote wa Elimu waliokuwa kwenye kikao
hicho wamesisitizwa kutumia nafazi zao
kuielimisha Jamii Juu ya umuhimu wa kupeleka watoto shuleni,kwani elimu ni kito
cha thamani,na daraja thabiti la kumvusha mwanadamu kutoka hatua moja ya chini
kwenda hatua nyingine ya mafanikio.
Post a Comment