Zaidi ya shilingi milioni 98 za kitanzania zimekusanywa
Zaidi ya
shilingi milioni 98 za kitanzania zimekusanywa katika zoezi la kuwasilisha zaka
kwa mwaka 2016, ambalo limefanyika leo katika kanisa kuu la mama mwenye huruma
la Ngokolo mjini Shinyanga.
Fedha hizo
ni zimetolewa na waamini kutoka jumuiya 64 kati ya 65 zinazounda parokia hiyo.
Makamu
mwenyekiti wa halmashauri walei parokia Bw.JOHN KAYOKA ameeleza kuridhishwa
kwake na mwitikio wa waamini katika utoaji wa zaka kwa mwaka huu kwani wameweza
kukusanya kiasi kikubwa cha fedha ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Amesema
fedha hizo zitatumika kwa ajili ya maendeleo ya kanisa na amewasitiza waaamini
kutochoka kuendelea kulitegemeza kanisa.
Akizungumza
mara baada ya kupokea zaka hizo,askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga Mhashamu
LIBERATUS SANGU amewashukuru waamini wote wa parokia ya Ngokolo kwa kutimiza
wajibu wao kikamilifu kwa ajili ya kulitegemeza kanisa.
Askofu SANGU
amesema kiasi cha fedha kilichopatikana
kinatokana na na moyo wa kujitoa sadaka kwa ajili ya kanisa bila kujali kipato hali
ambayo inaashiria uhakika wa waamini kuendelea kulitegemeza kanisa.
Post a Comment