Mwanamme raia wa Nigeria amenyongwa
Mwanamme raia wa Nigeria amenyongwa kwa kuhusika kwenye ulanguzi wa madawa ya kulevya baada ya kupatikana na kilo 2.6 za bangi.
Mwanamme huyo Chijioke Stephen Obioha wa umri wa miaka 38, alinyongwa leo katika gereza la Changi.
Obioha ambaye ana shahada ya kemia ya viwanda kutoka chuo cha Benin, alihamia nchini Singapore mwaka 2005, akiwa na matumaini ya kuwa mawanasoka.
Alikamatwa mwaka 2007 wakati alipatikana na misokoto 14 ya bangi ndani ya mkoba wake, na misokoto mingine 14 kweye nyumba alimokuwa akishi.
Chini ya sheria za Singapore, mtu yeyote ambaye atapatikana akiwa na zaidi ya gramu 500 za bangi anaweza kuhukumiwa kifo.
Kunyongwa kwa Obioha kunajiri baada ya kesi iliyochukua siku nyingi. Rufaa ya kwanza dhidi ya kesi hiyo ilitupiliwa mbali mwaka 2010.
Siku ya Alhamisi mawakili wake walikata rufaa ya mwisho ya kutaka hukumu hiyo ibadilishwe na kuwa kifungo cha maisha, lakini hilo lilikatiliwa na jopo la majaji watatu.
Kundi la haki za binadamu la Amnesty International limalaani hatua hiyo.
Singapore iliwanyonga watu wanne mwaka 2015, mmoja kwa makosa wa kuua na watatu kwa ulanguzi wa madawa ya kulevya, kwa mujibu wa takwimu za magereza.
Post a Comment