Header Ads

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akataza biashara barabarani


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo, amewataka wafanyabiashara wanaotumia maeneo ya waenda kwa miguu pembeni mwa         barabara za Manispaa ya Dodoma, kuondoa biashara hizo mara moja na kwenda maeneo waliyopangiwa rasmi.



Jafo ametoa agizo hilo katika ziara yake fupi ya kutembelea ujenzi wa maeneo mbalimbali ya mjini wa Dodoma ikiwa pamoja barabara ya kuelekea soko la majengo na dampo la kisasa la chidaye nje kidogo ya mji.
Amesema wafanyabiashara hao wanatakiwa kuondolewa na kupewa nafasi katika masoko rasmi kwani upangaji huo wa bidhaa pembeni ya barabara ni uchafuzi na uharibifu wa barabara, wakati mwingine husababisha ajali kutokana na waenda kwa miguu kukosa sehemu ya  kupita.

Kutokana na ujenzi wa barabara hiyo, wananchi pamoja na wafanyabiashara wa soko kuu majengo mkoani humo, wameanza kuondokana na adha ya muda mrefu ya ubovu wa miundombinu ya barabara kutokana na awali kutopitika na kutengeneza kwa kiwango cha lami, hali itakayosaidia kurahisisha usafiri wa abiria pamoja na mazao kuingia sokoni.
Mbali na ujenzi wa miundombinu ya barabara, lakini hivi sasa baadhi ya barabara za mji huo zinaendelea kukarabatiwa sambamba na ujengaji wa dampo la kisasa ikiwa ni maandalizi ya ujio wa makao makuu ya nchi.

No comments