Hali ya ubinafsi na kujali maslahi zaidi
Hali ya
ubinafsi na kujali maslahi zaidi imelezwa kuwa inachangia kwa kiasi kikubwa
kuendelea kwa vita na mafarakano katika maeneo mbalimbali duniani.
Akizungumza
katika misa ya kilele cha jubilee ya mwaka wa huruma ya Mungu, askofu wa jimbo
katoliki la Shinyanga mhashamu LIBERATUS SANGU amesema binadamu wameshindwa
kuwa chimbuko la amani kwa sababu ya kutawaliwa na hali ya maslahi binafsi,uchu
wa madaraka na ubinafsi
Akielezea
zaidi amebainisha kuwa, baada ya Mungu kumuumba binadamu alimwagiza kwenda
kuvitawala vitu vyote na kuvitiisha lakini ameshindwa kufanya hivyo na badala
yake kujikuta yeye mwenyewe akitawaliwa na kutishwa na vitu vya dunia kwa
kuendekeza tamaa za mali,madaraka na ubinafsi mambo ambayo yamesababisha
kuendelea kwa vita na mafarakano katika jamii.
Amewataka
wakristu kuungana kumwomba KRISTU autawale ulimwengu ili hali ya upendo na
amani iweze kurejea kwa vile binadamu wameshindwa kuwa chimbuko la amani na
utulivu.
Leo askofu
SANGU ameongoza misa takatifu ya kufunga jubilei ya mwaka wa huruma ya Mungu
katika kanisa kuu la mama mwenye huruma la Ngokolo mjini Shinyanga, misa ambayo
imekwenda sanjari na maadhimisho ya sikukuu ya KRISTU MFALME pamoja na zoezi la uwasilishaji wa zaka kiparokia.
Post a Comment