Header Ads

Serikali,wadau na viongozi wa dini wameshauriwa kutoa elimu zaidi kwa jamii ili iondokane na imani potofu


Image result for PICHA YA ALBINO


Serikali,wadau na viongozi wa dini wameshauriwa  kutoa elimu zaidi kwa jamii ili iondokane na imani potofu zinazochangia mauaji ya watu wenye ualbino.

Wito huo umetolewa leo na washiriki wa mdahalo wenye lengo la kupinga mauaji kwa watu wenye ualbino uliokuwa umeandaliwa na Radio Faraja kwa kushirikiana na shirika la THE FOUNDATION FOR CIVIL SOCIETY la jijini DAR-ES-SALAAM.
Washiriki wa mdahalo huo kwa pamoja wamesisitiza kutolewa kwa elimu zaidi katika jamii ili iwe na ufahamu kuhusu sababu za mtu kuzaliwa katika hali ya ualbino ili kuondoa mitazamo hasi kwa kundi hilo ambayo imekuwa ikisababisha baadhi ya watu kuamini kuwa viungo vyao vinaweza kuwasaidia kupata mafanikio.
                               
Pia wamependekeza jamii kushirikishwa kikamilifu katika suala la ulinzi na usalama hali ambayo itasaidia kuwabaini wanaojihusisha na mauaji hayo ikiwemo waganga wa kienyeji wanaopiga ramli chonganishi.

Naye mwakilishi wa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga SP.SHABU B.SHABU amesema jeshi hilo haliwezi kufanikiwa kukomesha mauaji hayo  peke yake, endapo jamii itaendelea kutotoa ushirikiano kwa kutoa taarifa za wahalifu wanaopanga mipango ya kufanya mauaji hayo na kutokuwa tayari kutoa ushahidi pale watuhumiwa wanapokamatwa. 

No comments