Header Ads

Zaidi ya shilingi milioni 98 za kitanzania zimekusanywa katika zoezi la kuwasilisha zaka kwa mwaka 2016, ambalo limefanyika leo katika kanisa kuu la mama mwenye huruma la Ngokolo mjini Shinyanga.
Fedha hizo ni zimetolewa na waamini kutoka jumuiya 64 kati ya 65 zinazounda parokia hiyo.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri walei parokia Bw.JOHN KAYOKA ameeleza kuridhishwa kwake na mwitikio wa waamini katika utoaji wa zaka kwa mwaka huu kwani wameweza kukusanya kiasi kikubwa cha fedha ikilinganishwa na mwaka uliopita.
Amesema fedha hizo zitatumika kwa ajili ya maendeleo ya kanisa na amewasitiza waaamini kutochoka kuendelea kulitegemeza kanisa.
Akizungumza mara baada ya kupokea zaka hizo,askofu wa jimbo katoliki la Shinyanga Mhashamu LIBERATUS SANGU amewashukuru waamini wote wa parokia ya Ngokolo kwa kutimiza wajibu wao kikamilifu kwa ajili ya kulitegemeza kanisa.

Askofu SANGU amesema  kiasi cha fedha kilichopatikana kinatokana na na moyo wa kujitoa sadaka kwa ajili ya kanisa bila kujali kipato hali ambayo inaashiria uhakika wa waamini kuendelea kulitegemeza kanisa.

No comments