Header Ads

UREMBO KUPEWA SAPOTI NA Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye

UREMBO KUPEWA SAPOTI NA Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye


TanzaniaImage copyrightGOOGLE
Image captionWaziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo nchini Tanzania Nape Moses Nnauye(kulia) akimkabidhi Bendera ya Tanzania Bi. Julietha Kabete(kushoto) Mrembo atakayeiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Afrika 2016 nchini Nigeria.

Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye , ameahidi kuendelea kufanya mageuzi makubwa katika mashindano ya urembo hapa nchini ili kuondoa dosari zinazojitokeza katika mashindano hayo.
Nape ametoa ahadi hiyo leo Jijini Dar es Salaam wakati akimkabidhi Bendera Mshiriki wa Tanzania katika mashindano ya urembo Bara la Afrika kwa mwaka 2016 yatakayofanyika Novemba 28 mwaka huu nchini Nigeria.
Nnauye ameongeza kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mashindano kama haya yanakuwa na tija Tanzania hasa katika kuleta ajira kwa vijana pamoja na kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo."Serikali nia yake ni kuhakikisha kuwa jambo hili linakuwa bora, linaminiwa na kuheshimika hivyo watanzania wote watajivunia uwepo wa mashindano ya urembo nchini" alisistiza Mhe Nnauye.
Aidha Mwakilishi wa Millen Magese group Ltd Bw. Matukio Aranyande Chuma amesema kuwa shindano hili litailetea sifa Tanzania na ni kwa mara ya kwanza kufanyika hivyo wataitumia fursa hiyo kuitangaza nchi kimataifa kupitia urembo.
Kwa upande wake Mshiriki kutoka Tanzania anayekwenda kushiriki mashindano hayo Bi. Julietha Kabete ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuunga mkono mashindano mbalimbali ya urembo Tanzania inaposhiriki."Naahidi kuitangaza nchi yangu vizuri katika mashindano haya na naomba watanzania waniombee na wanipigie kura ili niweze kushinda na kuitangaza Tanzania kimataifa katika urembo" Alisema Bi Julietha.
Mashindano ya Miss Afrika yameanzishwa mwaka 2016 na Prof. Bena Yage ambaye ni Gavana wa Jimbo la Cross River nchini Nigeria kwa lengo kupata mabalozi wa nchi za Afrika watakaosaidia kutangaza na kuelimsha waafrika kuhusu uchumi unaozingatia utunzaji wa mazingira.

1 comment: