MADEREVA WAOMBWA KUWA MAKINI BARABARANI ILI MKUPUNGUZA AJARI BARABARANI
Serikali imeombwa kuchukua hatua za kisheria dhidi ya madereva wanaotumia vilevi wakati wanapoendesha kwani wamekuwa wakisababisha ajali za mara kwa mara,
zinazopelekea vifo na majeruhi hali
ambayo inapunguza nguvu kazi ya Taifa.
Wakizungumza na redio faraja kwa nyakati tofauti baadhi ya
wakazi wa mji wa Shinyanga wamesema kuwa licha ya kuwepo sababu mbalimbali zinazopelekea ajali za barabarani
lakini matumizi ya vilevi hasa Pombe kwa baadhi ya madereva ni chanzo kikubwa
Wamezitaja sababu nyingine kuwa ni madereva kutozingatia
sheria za usalama barabarani,baadhi ya abiria wasiokuwa makini kuwashinikiza madereva waendeshe mwendo
kasi,lakini pia baadhi ya askari wa usalama barabarani kushindwa kuwajibika.
-
Baadhi ya madereva wametaja
baadhi ya mambo yanayochangia kutokea ajali kuwa ni
baadhi ya askari wa usalama
barabarani kuwa wasumbufu na kutokuwa
waaminifu hali inayowavuruga kisaikolojia.
Kwa upande wake mkuu wa Polisi kikosi cha usalama barabarani
Mkoa wa Shinyanga mrakibu wa Polisi ANTONY
MASANZU amesema Jeshi la Polisi lina wajibu mkubwa wa kuhakikisha
linasimamia sheria ya usalama barabarani ili kudhibiti ajali.
UZEMBE KWA BAADHI YA MADEREVA KUSHINDWA KUZINGATIA SHERIA,
KANUNI, NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI IMEELEZWA KUWA NI CHANZO CHA KUTOKEA
AJALI ZA MARA KWA MARA.
Post a Comment