Header Ads

Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amekatazwa


Mchungani wa Afrika kusini ambaye aliwapulizia dawa ya kuua wadudu inayoitwa Doom waumini amekatazwa

Lethebo Rabalago akimpulizia muumini DoomImage copyrightMOUNTZION GENERAL ASSEMBLY
Image captionLethebo Rabalago anadai dawa ya Doom inaweza kuwaponya watu saratani na HIV

Katika taarifa aliyoituma kwenye ukurasa wa Facebook, pmchungaji aliyejitangaza kama nabii Lethebo Rabalago alidai dawa ya kuua waduduinayojulikana kama Doom inaweza kuwaponya wengi.
Kampuni inayozalisha Doom imeonya juu ya hatari ya kupuliza dawa hiyo watu , huku tume maalum ya serikali ikimtaka yoyote atayeathirika kuwasilisha malalamiko.
Lakini mchungaji huyo ametetea kitendo hicho, akiiambia BBC kuwa anatumia mbinu zisizo za kawaida kuwaponya watu.
Muumini akipulizwa dawa ya DoomImage copyrightMZGA/FACEBOOK
Image captionMchungaji anadai waumini wamekuwa wakipona kwa kupulizwa dawa ya Doom
Nchi hiyo imekuwa na wimbila visa ambapo wajumbe wa kanisawamekuwa wakitendewa vitendo visivyo vya kawaida ili kupata tiba.
Katika picha zilizosambazwa kwenye kurasa za Facebook na Twitter, Bwana Rabalago, anayeendesha kanisa la Mountzion General Assembly katika jimbo la Limpopo ,anaeonekana akimpulizia dawa ya kuuwawadudu moja kwa moja kwenye macho yake na maeneo mengine mbali mbali ya mwili mbele ya waumini wa kanisa lake.
Amemueleza Nomsa Maseko aliyeko mjini Johannesburg kwamba alipuliza dawa hiyo kwenye uso wa mmoja wa wanawake kwasababu alikuwa na maambukizi ya macho na kudai kuwa "yuko sawa kwasababu anaamini nguvu za Mungu".
Pia alidai kuwa dawa hiyo ya Doom inaweza kuponesha saratani na virusi vya HIV vinavyosababisha.
Kampuni inayotengeneza dawa ya Doom kwa nembo ya Tiger inasema kuwa inamsihi s mchungaji aliyejitangazia kuwa ''nabii'' huko Limpopo - Lethebo Rabalogo kuacha kuwapuliza dawa ya wadudu kwenye nyuso za binadamu kama sehemu ya imani ya kuabudu:
Kopo la Doom
Image captionKampuni ya Tiger iko katika mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo
''Tunaona tendo hili kuwa kutia hofu kubwa , na tungependa kubainisha wazi kwamba ni hatari kupulizia Doom ama dawa nyingine yoyote ile ya wadudu kwenye macho ya watu''.
''Doom ilitengenezwa kwa ajili ya kuwauwa wadudu wa aina fulani ambao wameonyeshwa kwenye kopo , na maelezo yaliyoandikwa bayana kwenye kopo la Doom yameonya juu hatari na yanapaswa kufuatwa.''
''Kampuni ya Tiger iko katika mchakato wa kuwasiliana na Nabii kumtaka aache kufanya tendo hilo'' imesema kampuni ya Tiger.

chanzo bbc

No comments