Header Ads

Spika wa Bunge la Ulaya, Martin Schulz, ametangaza leo kuwa hatagombea muhula wa tatu


Image result for Spika wa Bunge la Ulaya, Martin Schulz


Spika wa Bunge la Ulaya, Martin Schulz, ametangaza leo kuwa hatagombea muhula wa tatu katika uchaguzi wa Januari. Schulz amewaambia waandishi wa habari mjini Brussels kuwa atarejea katika siasa za Ujerumani katika uchaguzi wa mwaka ujao. 

Mjerumani huyo amesema atagombea kiti cha bunge la Ujerumani kama kiongozi wa chama cha Social Democratic - SPD katika jimbo la North Rhine Westphalia.

 Schulz hakutoa maelezo zaidi katika kikao hicho cha habari kama atatafuta wadhifa wa waziri wa mambo ya nje au kugombea dhidi ya Kansela Angela Merkel katika uchaguzi wa bunge utakaoandaliwa Septemba mwaka ujao. 

Awali, uvumi kuwa Schulz, atajitosa tena katika siasa za Ujerumani uliongezeka baada ya serikali ya muungano kumuunga mkono mshirika wa chama cha Schulz, Frank-Walter Steinmeier kuwa rais ajaye wa Ujerumani. Vyombo vya habari vya Ujerumani vinamdokeza Schulz kuwa mrithi wa Steinmeier kama waziri wa mambo ya nje.

No comments