atanzania wameaswa kuitunza na kuidumisha amani iliyopo kwani ndiyo msingi thabiti wa mafanikio na maendeleo ya nchin
Watanzania wameaswa kuitunza 
na kuidumisha amani iliyopo kwani ndiyo msingi thabiti wa mafanikio na maendeleo
ya nchin
Wakizungumza na KALI ZOTE BLOG kwa nyakati tofauti baadhi ya
viongozi wa dini wa madhehebu mbalimbali mjini Shinyanga wamesema  moja ya wajibu wa viongozi wa dini ni
kuwahamasisha waumini wao kuitunza,na kidumisha amani   kupitia mafundisho kwenye nyumba za ibada
ili kuifanya nchi iendelee kuwa huru na salama
Wamesema  uhuru wa watu,maendeleo,usalama
wa nchi  na  hatua zozote za  mafanikio 
vinategemea zaidi hali ya amani na utulivu 
                                         -----
Kwa upande wake muinjilisti
marko Daud wa kanisa la k.k.k.t Ebeneza Shinyanga mjini amesema msingi wa
kuimarisha na kudumisha amani inahitaji kila mwananchi kutii,na kuheshimu
mamlaka  na sheria za nchi zilizopo,
kwani hata mafundisho na vitabu vitakatifu vinaelekeza hivyo.
                                          ---.
Wamesema watanzania wanapaswa kujifunza kutokana na mifano ya
nchi zenye vita,mizozo na migogoro ambapo 
hazina maendeleo kiuchumi,kisiasa,kiutaaduni  na kijamii,lakini pia watu wake hawana uhuru
wala amani. 
Post a Comment