Header Ads

MKUU wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwela, amewataka wavuvi kuzisalimisha ndani siku kumi.

MKUU wa Wilaya ya Busega mkoani Simiyu, Tano Mwela, amewataka wavuvi wanaotumia zana haramu katika kuvua samaki, kuzisalimisha ndani siku kumi.


Akizungumza na wavuvi katika Kijiji cha Nyamikoma kilichopo eneo la mwalo wa Fogofogo, Mwela alisema amewapa wavuvi hao siku kumi hadi Septemba 17 mwaka huu, vinginevyo watapambana na mkono wa sheria.
Wavuvi wa eneo hilo, wakiongozwa na Samwel Juma, walimuomba mkuu huyo wa wilaya, awaongeze muda wa siku za kuendelea na uvuvi, ili wapate mtaji wa kununua nyavu zinazokubalika za milimita nane.
Mwela alitupilia mbali ombi hilo la kutaka waongezewe muda wa mwezi mmoja ili wajipange kusalimisha na kununua nyavu zinazokubalika kisheria, akasema, hilo halikubaliki kwani limekuwa jambo la miaka mingi.

No comments