Waathiriwa wa tetemeko Bukoba, Tanzania waomba msaada
Waathiriwa wa
tetemeko la ardhi lililotokea mkoani Kagera kaskazini mwa Tanzania
Jumamosi wanaomba msaada ili kurejelea hali yao ya kawaida.
Watu 16 walifariki na wengine 250 kujeruhiwa kutokana na tetemeko hilo. Mamia wengine wamebaki bila makao.
Maafisa
wa serikali katika eneo hilo bado wanaendelea kutathmini maafa
yaliyosababishwa na tetemeko hilo la ukubwa wa 5.7 kwenye vipimo vya
Richter.
Tetemeko hilo limetajwa kuwa mbaya zaidi kuwahi kukumba taifa hilo la Afrika Mashariki katika kipindi cha zaidi ya mwongo mmoja.
Tetemeko
hilo, ambalo kitovu chake kilikuwa kilomita takriban kilomita 44 kutoka
mji wa Bukoba, mji mkuu wa mkoa wa Kagera kwa mujibu wa taasisi ya
jiolojia ya Marekani.
Mitetemeko ilisikika maeneo ya Uganda, Kenya, Rwanda na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Mji huo, wenye wakazi 70,000, uliathirika pakubwa.
Kufikia Jumatatu, waathiriwa walionekana kwenye vifusi vya majumba yao yaliyoporomoka wakijaribu kuokoa mali yao.
Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, aliyetembelea mji wa Bukoba, ameagiza baraza la
mji huo kufanya utathmini kubaini uharibifu uliotokea na kupendekeza
jinsi serikali kuu inaweza kusaidia.
Rais wa Tanzania Dkt John
Pombe Magufuli ameahirisha ziara ya siku tatu nchini Zambia ambapo
pamoja na mambo mengine alikuwa ahudhurie sherehe za kuapishwa kwa Rais
Edgar Chagwa Lungu ili aweze kushughulikia tatizo la tetemeko hilo.
Rais Magufuli amemtuma Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kumuwakilisha.
Rais wa nchi jirani ya Kenya Uhuru Kenyatta
amezungumza kwa njia ya simu na Rais Magufuli kumpa pole zake na
akaahidi kutoa usaidizi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa msemaji wa Rais Kenyatta, Kenya itatoa msaada wa mabati, blanketi na magodoro.
Msaada
huo utasafirishwa kwa ndege na jeshi la Kenya kesho Jumanne hadi maeneo
yaliyoathiriwa nchini Tanzania, taarifa hiyo imesema.
Post a Comment