Juhudi za kukabiliana na vitendo vya ukeketaji zinazofanywa na wadau mbalimbali katika wilaya ya Tarime mkoani Mara
Juhudi za kukabiliana na vitendo vya ukeketaji zinazofanywa na wadau mbalimbali katika wilaya ya Tarime mkoani Mara
Juhudi za kukabiliana na vitendo vya ukeketaji zinazofanywa
na wadau mbalimbali katika wilaya ya Tarime mkoani Mara zimekuwa hazifikii
malengo yaliyokusudia kutokana na mila hizo kuchukuliwa kama chanzo cha
kujiingizia kipato.
Hayo yamebainishwa na mkurugenzi wa Shirika la
ATFGM Bw. VARELIAN MGANI ambaye shirika
lake linatkeleza mradi wa kuzia vitendo vya ukeketaji kwa watoto wa kike katika
wilaya hiyo.
Akizungumza katika kikao cha kubadilishana
uzoefu na shirika la AGAPE la mjini Shinyanga ambalo linaendesha mradi wa
kuzuia mimba na ndoa za utotoni Bw.MGANI amebainisha kuwa juhudi wanazozifanya
za kuzuia ukeketaji zinakumbana na changamoto kubwa kutoka kwa viongozi wa
kimila na Mangariba ambao wanalipwa ujira mkubwa kutokana na kzi hiyo.
Kwa upande wake mwanasheria wa shirika hilo BI. IRENE THOMAS amezitaja changamoto nyingine zinazowakabili ni kukosa ushirikiano
kwa jamii katika kesi zinawakabili wanaojiusisha na vitendo vya ukeketaji ikiwemo zile zinazohusu ndoa za mimba za
utotoni..
Shirika la ATFGM la mkoani MARA ambalo liko
chini ya kanisa Katoliki na shirika la
AGAPE ala mjini Shinyanga kwa pamoja yanatekeleza miradi mbalimbali yenye lengo
la kumkomboa motto wa kike kwa kuhakikisha yanaondoa vikwazo vyote
vinavyomfanya asipige hatua.
Post a Comment