Header Ads

mke wa rais wa tanzania ameruhusiwa muhimbili


Mshirikishe mwenzako

Magufuli akimjulia hali mkewe hospitaliniImage copyrightIKULU, TANZANIA

Mke wa Rais wa Tanzania John Magufuli, Janeth, aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili ameruhusiwa kuondoka hospitalini.
Ikulu ilitoa picha ya Rais Magufuli akimjulia hali katika wodi ya Sewa Haji Alhamisi ingawa haikusema alikuwa anaugua wapi.
Taarifa nyingine iliyotolewa na ikulu Ijumaa imesema ameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya afya yake kuimarika na akarejea nyumbani.
Ikulu imesema Mama Janeth Magufuli alilazwa hospitalini Jumatano baada ya "kuugua ghafla na kupoteza fahamu".
"Namshukuru sana Mungu kwamba afya yangu imeimarika, pia napenda kuwashukuru Madaktari na Wauguzi, nimepata huduma nzuri sana maana siku nilipoletwa hapa nilikuwa sina fahamu na hali yangu ilikuwa mbaya lakini mmenipigania na leo narudi nyumbani nikiwa na afya imara," alisema kabla ya kuondoka hospitalini.
"Naomba pia niwashukuru Watanzania wote kwa kuniombea, nawahakikishie kuwa sasa nipo vizuri na madaktari wameniruhusu nirudi nyumbani ambako nitamalizia matibabu yangu."
Novemba mwaka jana, siku chache baada ya kuapishwa hospitali hiyo ni miongoni mwa taasisi za serikali ambapo Rais Magufuli alifanya ziara ya kushtukiza.
Alisema alisikitishwa na kuhuzunishwa na hali ya huduma kwa wagonjwa hususan wanaolala chini.

Magufuli akimjulia hali mkewe hospitaliniImage copyrightIKULU, TANZANIA
Image captionMagufuli akimjulia hali mkewe hospitalini

Aidha, alikuta baadhi ya vifaa vya kufanyia kazi na mashine muhimu za uchunguzi wa magonjwa kama vile MRI na CT-SCAN vikiwa havifanyi kazi kwa muda wa miezi kadhaa.
Alibadilisha usimamizi wa hospitali hiyo.
Taarifa ya ikulu ilisema Alhamisi, Rais Magufuli alipofika kumjulia hali mkewe, wagonjwa waliolazwa katika wodi ya Sewa Haji walimshukuru "kwa hatua zilizochukuliwa na serikali kuboresha hospitali ya taifa ya Muhimbili na wamebainisha kuwa licha ya kuboreshwa kwa mazingira ya hospitali, pia wanapata huduma nzuri kutoka kwa madaktari na wauguzi."

No comments