waandishi wa habari singida wa nusilika kufa
Jeshi la Polisi Mkoani
Singida linawashikilia watu wawili kwa kuwatishia kuwaua kwa risasi
waandishi wa habari mkoani humo ambao walitoa taarifa kwenye vyombo vya
habari kuhusu tukio la wizi na udhalilishaji lililofanywa na watuhumiwa
hao.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mayala Towo.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida Mayala Towu amewataja
watuhumiwa hao ambao ni Hussein na Hassan ambao wanadaiwa kuvamia katika
ofisi ya chama cha waandishi wa mkoa wa Singida na kutoa maneno ya
vitisho kwa waandishi hao.
Watu hao wanadaiwa kuwa waliwaambia waandishi hao kama wataendelea
kutoa taarifa zao basi watawadhuru wao na familia zao ndipo waandishi
hao walipochukua hatua ya kuripoti tukio hilo polisi na hatimaye
watuhumiwa hao kushikiliwa na jeshi la polisi.
Kamanda Mayala amesema kuwa baada ya kuwashikilia watu hao walifanya
msako katika makazi yao na kuwakuta na bunduki mbili aina ya rifle hivyo
waliwashikilia kwa muda na kuwafungulia kesi ili kujibu tuhuma hizo.
Post a Comment