mtaa wa dome atalini msim huu wa mvua
Wakazi wa mtaa wa Dome
kata ya Ndembezi katika Manispaa ya Shinyanga wametakiwa kuweka
mazingira yao katika hali ya usafi,ili kuchukua tahadhari ya magonjwa ya mlipuko katika kipindi hiki cha
masika.
Akizungumza na redio faraja
ofisini kwake mwenyekiti wa
serikali ya mtaa wa Dome Solomon Nalinga amesema katika kipindi
hiki ambacho mvua za masika zimeanza kunyesha,ni vyema wananchi kuchukua
tahadhari dhidi ya magonjwa ya mlipuko .
--
Mwenyekiti huyo amesema kiongozi bila kuwa na utashi wa kazi
ni chanzo cha kutengeneza mazingira magumu kiusalama,na kwamba Ili Nchi iweze kupiga hatua ya mafanikio na maendeleo viongozi na watendaji kuanzia ngazi ya serikali za mitaa wanapaswa
kuwa na utashi wa kazi na uwajibikaji kwa
maslahi ya Jamii
Ametoa wito kwa Jamii hususani vijana kufanya kazi kwa bidii
badala ya kuzurura,kutumia vilevi na kufanya uhalifu.
Bwana NALINGA ametumia fursa hiyo kukumbusha
wajibu wa viongozi wa serikali za mitaa,vijiji na vitongoji
kushirikiana na serikali kuu kutengeneza
mazingira salama ya Jamii ili ipende kufanya
kazi na shughuli halali kwa lengo la kujipatia
kipato,ikiwa ni Pamoja na kudhibiti uhalifu
Post a Comment