wana kijiji wa seseko kulia machozi ya dam
wana kijiji wa seseko kulia machozi ya dam
Baadhi ya wakazi wa kijiji cha Seseko kilichopo katika Kata
ya Mwamalili Manispaa ya Shinyanga wamewalalamikia viongozi kushindwa kuweka
mgawanyo sawa wa huduma za kijamii,kwani huduma nyingi zimeelekezwa zaidi katika kijiji Jirani cha
Mwamalili
Wakizungumza na redio faraja fm stereo kwa nyakati tofauti
wamesema kijiji cha Seseko kinakabiliwa na ukosefu wa huduma za kijamii ikiwemo
maji,barabara,na zahanati hali inayowakatisha tamaa na kuwafanya wakose imani
kwa serikali yao.
Wamelalamia pia kutokamilika
ujenzi wa Jengo la Zahanati ambapo
ni muda mrefu sasa tangu kuanza kwa
ujenzi wake,hali inayowalazimu kufuata huduma za afya katika vijiji Jirani
Kwa upande wake mwenyekiti wa serikali ya kijiji cha Seseko EZEKIEL MABULA amekiri kuwepo
changamoto hizo na kusema kuwa tayari wamefikisha kwenye uongozi wa ngazi za
Juu akiwemo diwani,na kwamba wananchi waendelee kushirikiana kuishinikiza
serikali ili waweze kupata ufumbuzi wa kero hizo.
Wananchi hao wameiomba serikali kukisikia kilio chao na kisha
kutafuta ufumbuzi ili kuwawezesha kupata huduma hizo ambazo ni stahiki kijamii.
Post a Comment