TANZANIA YA ZIDI KUPINGA ATUA ZAIDI
TANZANIA YA ZIDI KUPIGA ATUA ZAIDI
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na watoto Ummy Mwalimu mapema leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar Abdullah Al Maadadi ofisini kwake na kuzungumza kuhusu masuala mbalimbali yanayohusu sekta ya afya.Watoto Mhe. Ummy Mwalimu akizungumza na Balozi wa Qatar nchini Tanzania Abdullah Al Maadadi.
Katika mazungumzo yao yaliyofanyika ofisi za wizara hiyo Jijini Dar
es salaam Waziri Mwalimu amesema kuwa Qatar imeonesha nia ya kuendelea
kushirikiana na Tanzania kwaajili ya kutatua matatizo mbalimbali
yaliyopo kwenye sekta ya afya hasa maeneo ambayo bado hayajafikiwa na
huduma za uhakika za afya
Amesema katika mazungumzo na balozi huyo wamekubaliana kuanza
mchakato wa kuwa na makubaliano ya mahusiano rasmi kwa kusaini hati ya
makubaliano ambayo yataweka wazi maeneo ya ushirikiano kati ya Qatar na
Tanzania.
Kwa upande wa Qatar wameonyesha nia ya kuisaidia nchi katika kutoa
vifaa tiba kwaajili ya hospitali na kwa sasa tayari wizara hiyo imepokea
magari 10 ya wagonjwa kutoka Qatar na taratibu za kuyatoa bandarini
zinakamilishwa na zitapelekwa katika halmashauri mbalimbali ambazo
hazina magari.
Kwa upande wake Balozi wa Qatar Abdullah Al Maadadi amekubali
kuisaidia Tanzania katika kuleta vifaa tiba na kufanya ujenzi kwa baadhi
ya wilaya nchini ambazo mapato yake bado ni kidogo hayawezi kukidhi
gharama za ujenzi wa hospitali na vituo vya afya sambamba na kuleta
wataalamu wa matibabu ya upasuaji wa moyo wataalamu ambao watashirikiana
na wataalamu wa taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete ya
Post a Comment