Vikundi vya ujasiriamali vimeshauriwa kuondoa itikadi za kivyama na kidini ilikuweza kupiga hatua katika kuleta maendeleo
Vikundi vya ujasiriamali vimeshauriwa kuondoa itikadi za kivyama na kidini ilikuweza kupiga hatua katika kuleta maendeleo
Vikundi vya ujasiriamali vimeshauriwa kuondoa
itikadi za kivyama na kidini ilikuweza kupiga hatua katika kuleta maendeleo
.
Akifunga warsha fupi ya kusoma mapato ya kikundi cha
ujasiriamali ambacho kinajishughulisha na ulimaji wa mbogamboga katika kijiji
cha Nhelegani manispaa ya shinyanga mwenyekiti wa kijiji hicho Seni Shija amewaomba
wanakikundi kuondoa itikadi za kisiasa na imani za kidini ili kuondoa tofauti
katika kuleta maendeleo.
Mwanzo wakati kikundi hicho kikisoma risala yake
mbele ya mgeni kimesema kuwa kikundi kinakabiliwa na changamoto kama ukosefu wa
elimu ya ujasiriamali kwa wakulima, upungufu wa mtaji kwa wakulima na vitendea
kazi kwa ujumla.
Diwani wa kata ya kizumbi bwana Ruben Kitinya ambaye
alikuwa ndiye mgeni rasmi amewapongeza wanakikundi hao kwa hatua ambayo
wameweza kufikia hivi sasa na kuweza kutoa ahadi ya kushirikiana nao ,ikiwa
pamoja na kuleta wataalamu wa elimu ya ujasiriamali na kufanya marekebisho
katika visima vya maji ambavyo ni vibovu.
Naye mwenyekiti wa kikundi hicho ndugu Mbogo Mustafa
Sombi ameisihi serikali ya awamu ya tano na jamii kwa ujumla kuvikumbuka vikundi
vidogovidogo vya ujasiriamali pindi vinapohitaji msaada.
Post a Comment