Header Ads

viongozi watatu wa chadema wa shikiliwa na polisi tabora

viongozi watatu wa chadema wa shikiliwa na polisi tabora
Image result for PICHA YA chadema
JESHI la polisi wilaya ya Igunga mkoani Tabora limewashikilia  na kuwafikisha mahakamani viongozi watatu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa tuhuma za kufanya mkusanyiko usiokuwa halali.

Waliofikishwa katika mahakamani ya hakimu mkazi ni Katibu wa chama hicho wilaya ya Igunga, Idd Ndagwemeleye (54) mkazi wa mtaa wa Mwayunge, Aluhanya Ngozo (48) mkazi wa kitongoji cha Mwamsunga ambaye ni katibu wa tawi katika kitongoji hicho na Fea Lipa (41) mkazi wa Mwamsunga ambaye ni Mwenyekiti wa tawi la Mwamsunga.

Aidha, mwendesha mashitaka wa jeshi la polisi wilaya ya Igunga, Elimajid Kweyamba aliiambia mahakama jana mbele ya hakimu wa wilaya, Ajali Millanzi kuwa washtakiwa hao walitenda kosa hilo, Oktoba 30, mwaka huu, kuanzia saa nne asubuhi hadi saa 12 jioni katika kitongoji cha Mwamsunga.
Alidai washtakiwa wote kwa pamoja wakiwa wafuasi na viongozi wa Chadema walifanya mkusanyiko usiokuwa halali ambao ungeweza kusababisha uvunjifu wa amani.
Aidha, alisema washitakiwa wote hao wanatuhumiwa kutenda kosa hilo kinyume na kifungu 74 na 75 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 marekebisho ya mwaka 2002 inayozuia kutenda makosa kama hayo.
Baada ya kusomewa mashtaka yao, washitakiwa wote walikana kutenda makosa hayo na kesi hiyo imeahirishwa hadi Novemba 10, mwaka huu, itakapotajwa tena na washitakiwa wote wako nje kwa dhamana ya Sh 700,000 kila mmoja.

Mahakama hiyo imepiga marufuku kwa muda usiojulikana kwa viongozi hao kufanya mikutano isiyoruhusiwa kisheria hadi kesi yao iliyopo mahakamani itakapokwisha.

No comments