Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema siku akiletewa Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari atausaini muda huo huo ili uanze kufanya kazi mara moja.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli
amesema siku akiletewa Muswada wa Sheria ya Vyombo vya Habari atausaini
muda huo huo ili uanze kufanya kazi mara moja.
Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari Ikulu jijini Dar
es salaam, Rais Magufuli amesema hawezi kuzungumza lolote kuhusu muswada
huo kwa kuwa muswada huyo utajadiliwa bungeni na wabunge wote.
“Kuniambia mambo ya bunge ambayo bado sijaletewa, utakuwa unanionea
katika utawala wa bunge,” Magufuli alimjibu mwandishi aliyehoji kuhusu
muswada huo. “Tuwaache wabunge watimize wajibu wao. Sasa unaponiambia
ukiletwa niikatae nataka nikueleze bila unafiki siku utakapo fika siku
hiyo hiyo nitausaini, ili msubiri kama utakuja wakati mwingine mje
muubadilishe, sitaki kufrastuate mambo ya bunge,”
Aliongeza, “Lakini lazima tukubali kwamba hii sheria imechelewa, na
unakuta mnazungumza kwa lugha ya wamiliki fulani fulani. Lakini muswada
huu sifahamu wabunge watakacho amua lakini niya ni kulinda waandishi wa
habari,”
Katika hatua nyingine Rais Magufuli amewataka watanzania kufanya kazi kwa bidii ili wapate kipato kutokana na kazi wanazofanya.
“Tanzania ni tajiri, kinachotakiwa ni namna ya kubalance rasilimali,
katika kufanya hilo mimi nimeamua kubana matumizi serikalini kwa mfano
nimedhibiti safari za nje kwa kuanza na mimi mwenyewe, tangu niingie
madarakani nimepata mialiko 47 lakini nimekwenda mialiko mitatu.”
Alisema Rais Magufuli.
Post a Comment