Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, amesema serikali inatambua umuhimu wa askari polisi
Waziri wa mambo ya ndani, Mwigulu Nchemba, amesema serikali inatambua umuhimu wa askari polisi na ndio maana ina mkakati wa kuliwezesha jeshi hilo vitendea kazi bora.
Waziri Nchemba ameyasema hayo Jumatano hii alipokuwa akitoa ufafanuzi wa matukio ya kuvamiwa kwa askari kujeruhiwa au hata kuuawa.
“Serikali inatambua umuhimu wa askari polisi, wanapokuwa katika kutimiza majukumu yao ya kila siku. Napenda kulihakikishia bunge lako tukufu kwamba serikali itaendelea kuliwezesha jeshi la polisi hapa nchini kwa vitendea kazi bora na kuwajengea uwezo askari wetu kwa mafunzo ili waweze kukabiliana na matukio ya uhalifu yanayohusisha uvamizi wa askari polisi,” alisema Nchemba.
“Kwa sehemu ya pili jeshi la polisi limefanikiwa kukamata silaha 19 kati ya 23 zilizoporwa kutoka kwa askari waliovamiwa wakiwa katika majukumu yao katika kipindi cha Julai 2015 hadi Septemba 2016,” aliongeza.
Post a Comment