alubino mkoa shinyanga waomba ulinzi
alubino mkoa shinyanga waomba ulinzi
Baadhi ya
watoto wenye ualbino wanaolelewa katika kituo cha Buhangija mjini Shinyanga
wameitaka serikali kuweka utaratibu wa kuwachukulia hatua viongozi wa maeneo
yanakotokea mauaji ya watu wenye ualbino,kama njia ya kuwashinikiza kuweka
mikakati ya kudhibiti mauaji hayo katika maeneo yao.
Wakizungumza
na radio faraja katika kituo hicho watoto hao wamesema haiwezekazi wauaji
watoke maeneo ya mbali bila kuwepo ushiriki wa watu wa karibu hali ambayo ingeweza
kudhibitiwa kama viongozi wa maeneo husika wangeweka mikakati ya kuwalinda watu
wenye ualbino waliopo katika maeneo yao.
Watoto hao
pia wameiomba serikali kwa kushirikiana na wadau kuendelea kutoa elimu kwa jamii
kuhusu watu maana ya ualbino ili kuondoa imani potofu ambazo zimejengeka
miongoni mwa jamii kuwa viungo vyao vinaweza kusaidia kupata utajiri.
Kituo cha
watoto wenye mahitaji maalum cha Buhangija,hivi sasa kinalea watoto wenye
ualbino zaidi ya 200 ambao wamelazimika kuzikimbia familia zao kwa hofu ya
kuuawa na watu wanaotafuta viuongo vyao.
Post a Comment