Header Ads

Kanisa linalotumiwa na watu weusi kuteketezwa kwa moto

Kanisa linalotumiwa na watu weusi kuteketezwa  kwa moto  

Kanisa la Hopewell

 Polisi katika jimbo la Marekani la Mississippi  wanachunguza uhalifu wa chuki baada ya Kanisa linalotumiwa na watu weusi kuteketezwa  kwa moto  kisha kuchorwa maneno ya kusema: "Mpigie kura Trump".


Kanisa hilo linalopatikana eneo la Greenville lilijengwa miaka 111 iliyopita.

Msimamizi wa kituo cha zima Moto alisema kuwa moto katika Kanisa la Hopewell Missionary Baptist Church uliwashwa makusudi.

Shambulio hilo limetokea wiki moja kabla ya uchaguzi wa urais kufanyika Jumanne wiki ijayo.
Maafisa wanasema ujumbe ulioandikwa kwenye jumba hilo ni wa kuzua hofu.

Meya wa Greenville, Mississippi amesema kisa hitendo hicho ni cha "chuki na woga" na s"shambulio la moja kwa moja dhidi ya uhuru wa watu kuabudu".

Kisa hicho kinawakumbusha watu kuhusu visa vya kuchomwa moto kwa makanisa ya watu weusi miaka ya 1950 na 1960, watu weusi waliokuwa wanapigania haki zao.

Maafisa wa FBI wakishirikiana na wachunguzi wa jinai wa jimbo la Mississippi kwa sasa wanaendelea na uchunguzi.

No comments