Bashe ametoa kauli hiyo katika jukwaa la CCM wakati akimuombea ridhaa mgombea 
wao Maulid Mtulia ili aweze kuwa muwakilishi wa Jimbo la Kinondoni katika siku zijazo
 endapo atapata kura nyingi za ndio siku ya kupiga kura ambapo mpaka sasa zimebakia
 takribani siku mbili. 
"Naviomba vyombo vya ulinzi na usalama, vifanye kila jitihada kufanya 
uchunguzi wa kina ili aliyefanya uhalifu huu aweze kupatikana. Kumekuwa na
 tabia kila uchaguzi mdogo unapofanyika matendo ya kihalifu hufanyika halafu 
wenzetu wa upande wa pili huamishia kesi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM)", 
amesema Bashe.
Pamoja na hayo, Bashe ameendelea kwa kusema "jambo hili lililotokea Jimbo la
 Kinondoni ni kulaaniwa, sisi tunalilaani na nyie wananchi wa Kinondoni
 muendelee kulilaani lakini tuombe ufanyike uchunguzi na anayehusika
 apelekwe kwenye vyombo vya dola, ashtakiwe na watanzania tuambiwe ni
 nani anayehusika na tukio hili".
Kwa upande mwingine, Kamanda wa Polisi Kinondoni Murilo Jumanne Murilo (jana) amesema Jeshi lake litachunguza kifo cha Kiongozi wa CHADEMA kata ya Hananasif, ambaye mwili wake uliokotwa ukiwa na majeraha kwa kufuata misingi ya kazi yao na siyo kusukumwa na hisia za mtu binafsi.