Liverpool inajiandaa kwa jaribio la pili kumsajili kiungo wa wakti wa Monaco mwenye umri wa miaka 22 T
Liverpool inajiandaa kwa jaribio la pili kumsajili kiungo wa wakti wa Monaco mwenye umri wa miaka 22 Thomas Lemar wa Ufaransa baada ya kukataa kandarasi mpya katika klabu hiyo ya ligi ya daraja la kwanza.
Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola hatoanzisha tena harakati za kutaka kumsajili winga wa Leicester raia wa Algeria mwenye umri wa miaka 26 Riyad Mahrez mwishoni mwa msimu huu. (mirror)
Mkufunzi wa zamani wa Barcelona Luis Enrique ambaye anahusishwa na kuchukua mahala pake Antonio Conte wa Chelsea anajiandaa kuelekea nchini Uingereza.
Hatahivyo mkufunzi huyo mwenye umri wa miaka 47 hataki kumrithi Conte hadi mwisho wa msimu huu.
Obrey Chirwa amempiku John Bocco katika harakati za kushinda taji la mfungaji bora katika Ligi Kuu Bara, Lakini Okwi bado ndiye aliye juu kwa mabao.
Chirwa aliyeanza wiki akiwa na mabao sawa na mshambuliaji wa Simba alifunga hat-trick kaytika mchuano kati ya yanga na Njombe mji katika uanwja wa kitaifa.
Tottenham inataka kumsaini kiungo wa kati wa Watford na Ufaransa Abdoulaye Doucoure mwishoni mwa msimu huu.
Beki wa Brazil Fabinho mwenye umri wa miaka 24 ambaye klabu ya Manchester United ilikuwa inamnyatia msimu uliopita anasema kuwa muda wake katika klabu ya Monaco unakamilika(Metro)
Post a Comment