Klabu ya Liverpool itaangalia uwezekano wa kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere
Klabu ya Liverpool itaangalia
uwezekano wa kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere
Klabu ya Liverpool itaangalia
uwezekano wa kumsajili kiungo wa Arsenal Jack Wilshere, kama mchezaji
huyo atagoma kusaini mkataba mpya na klabu yake.
Manchester United
wanamfutilia kwa karibu kiungo wa Real Madrid Mateo Kovacic ili kuweza
kumsajili kiungo huyo katika dirisha kubwa la usajili.
Mshambuliji
wa Man United Marcus Rashford anaweza kuondoka klabuni hapo ikiwa
United wa tamsajili Justin Kluiverts kutoka Ajax.
Mshambuliaji wa Kibrazil Malcom Oliveira, anataka kuondoka katika
klabu yake ya Bordeaux, na Mchezaji huyo anawinda na Tottenham na
Arsenal
Mshambuliji wa West Ham Javier Hernandez, 29, amesema
atajitoa kwa asilimia mia moja katika klabu yake licha ya kutaka
kuondoka klabuni hapo katika dirisha la mwezi januari
Mfaransa
Olivier Giroud mwenye miaka 31 ambae anaweza anza katika mchezo wa timu
yake mpya ya Chelsea itapocheza na Watford amesema alipewa motisha ya
kuhama na kocha wa timu ya taifa ya ufaransa Didier Deschamps.
Winga wa Leicester Marc Albrighton amekanusha taarifa zinazozagaa
mitandaoni kuwa wachezaji wa Foxes wanahasira na mchezaji mwenzao
Riyad Mahrez aliyetaka kuhama na kujiunga na Man City.
Meneja wa
Manchester United hana mpango wa kumsajili mchezaji wa idara ya
ushambuliaji katika dirisha lijalo la usajili kwa kuwa ana furaha na
ukubwa kikosi alichonacho.
Kiungo wa Chelsea Danny Danny
Drinkwater amesema mchezaji mwenzake Eden Hazard na Paul Scholes ndio
wachezaji bora aliwahi kucheza nao.
Post a Comment