Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Magufuli leo Februari 1, 2018 amemtolea uvivu hadharani Waziri wa Katiba na Sheria
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt. John Magufuli leo Februari 1, 2018 amemtolea uvivu hadharani Waziri wa Katiba na Sheria, Prof. Palamagamba Kabudi kuwa na yeye na Mwanasheria Mkuu wa Serikali wanakwamisha haki kutendeka kwa watu kutokana na kutofanyia kazi mambo mengi ya msingi.
Rais Magufuli amesema hayo leo jijini Dar es salaam alipokuwa akihutubia kwenye maadhimisho ya kilele cha wiki ya sheria na kusema kuwa yeye ni mtu aliyeumbwa kusema na ataendelea kusema ukweli hadharani hata kama kuna watu anawaumiza.
“Kinachoshangaza pamoja na hatua nzuri ya Serikali kupeleka hhi Legal Aid Act ya mwaka 2017 na mapendekezo mbalimbali kwa ajili ya kuwasaidia wananchi lakini ‘regulation’ mpaka sasa hivi hazijaletwa ila Waziri yupo tena Mwanasheria, tena ni Profesa, AG yupo, Deputy AG yupo jamani mtanisamehe sana mimi ndivyo nilivyo nawasema hapa hapa kwa hiyo wewe Profesa Juma na majaji na mahakimu hamna ‘Instrument’ za kuweza kutoa uamuzi. Wabunge wao wamepitisha sheria, mimi nikaletewa nikasaini lakini regulations mpaka leo miezi mingapi imepita? miezi tisa. Watu wapo wanakula tu mishahara, magari wanayo na viyoyozi vipo ila wananchi wanapata shida na muda mwingine mtasingiziwa mahakama kwamba hamtoi haki kumbe ni Serikali watendaji wake hawatoi haki kwa Watanzania,” amesema Rais Magufuli.
Post a Comment