Header Ads

Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Saudi Arabia Adel aj-Jubeir amesema kuwa nchi hiyo haitaathirika na uamuzi wa Ujerumani


Image result for Kigeni wa Saudi Arabia Adel aj-Jubeir


Waziri wa Mambo ya Kigeni wa Saudi Arabia Adel aj-Jubeir amesema kuwa nchi hiyo haitaathirika na uamuzi wa Ujerumani kusitisha uuzaji wa silaha katika nchi 
zinazohusika na vita vya Yemen. 

Al-Jubeir amesema inashangaza kuwa Ujerumani inaonekana kubagua katika kile inachokiuza na isichokiuza wakati kuna vita vya halali, na hilo halisaidii katika kuonyesha hali ya kuaminika kwa serikali ya Ujerumani.

 Mnamo mwezi Januari, Ujerumani ilisema itasitisha uuzaji wa silaha katika nchi zinazohusika katika mgogoro wa Yemen. Saudia na Umoja wa Falme za Kiarabu ni miongoni mwa nchi 10 zilizonunua silaha kwa wingi kutoka Ujerumani katika mwaka wa 2017.

 Muungano wa nchi za Kiarabu umekuwa ukipigana nchini Yemen dhidi ya waasi wa Houthi wa madhehebu ya Shia tangu mwaka wa 2015. Muungano huo unajumuisha nchi kama Misri, Jordan, Bahrain, Kuwait na Umoja wa Falme za Kiarabu.

No comments