Uwanja wa ndege wa mjini London umefungwa
Uwanja wa ndege wa mjini London umefungwa baada ya bomu la vita vya pili vya dunia kupatikana kwenye mto ulio karibu wa Thames.
Uwanja huo utafungwa siku nzima na safari zote za ndege kufutwa, na kuwaathiri hadi abiria 16,000.
Bomu hilo liligunduliwa siku ya Jumapili eneo la George V wakati wa shughuli ya kikazi mashariki mwa London.
Uwanja huo ukafungwa na polisi wanasema kuwa wanashirikiana na jeshi la wanamaji kuondia bomu hilo.
Abiria wameambiwa wasisafiri kwenda uwanja huo na kushauriwa kuwasiliana na mashirika yao ya ndege.
"Uwanja wa ndege unashirikiana kabisa na polisi wa Met na jeshi la wanamaji kuliondoa bomu hilo kwa njia salama na kutatua suala hilo haraka iwezekanavyo," alisema Robert Sinclair, mkurugenzi mkuu wa uwanja huo.
Ndege zinazotumia uwanjai huo wa London City ni pamoja na British Airways, Flybe, CityJet, KLM na Lufthansa kwa safari za ndani na kwenda nchi zingine zaUlaya.
Post a Comment