Header Ads

Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema picha za satelaiti zinaonyesha kuwa vikosi vya Myanmar vimeharibu vijiji 55

Image result


Shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema picha za satelaiti zinaonyesha kuwa vikosi vya Myanmar vimeharibu vijiji 55 vya Warohingya katika eneo la kaskazini mwa jimbo la Rakhine katika miezi ya karibuni. 

Shirika hilo limeilaani serikali ya Myanmar kwa kile ilichosema ni kufuta ushahidi katika maeneo ambayo wanajeshi wanatuhumiwa kufanya maovu. Maeneo ya kaskazini mwa jimbo la Rakhine yamebaki bila wakaazi wa Rohingya tangu Agosti mwaka jana, wakati ukandamizaji wa kijeshi uliposababisha kukimbia karibu watu 700,000 wa jamii hiyo ya walio wachache. 

Wengi wao walilazimika kuvuka mpaka na kuingia Bangladesh. Human Rights Watch imesema maovu mengi yalitekelezwa katika vijiji hivyo na vilistahili kuhifadhiwa ili wataalamu walioteuliwa na Umoja wa Mataifa waweze kuorodhesha unyanyasaji uliofanywa na kuchunguza ushahidi kwa makini kwa ajili ya kuwatambua waliohusika.

No comments