Kamishna mahakamani kwa sakata la Tanzanite
Kamishna mahakamani kwa sakata la Tanzanite
Kaimu kamishna wa madini na Katibu wa Bodi ya Ushauri katika sekta ya Madini, Ally Samanje amefikishwa mahakamani Kisutu, jijini Dar es Salaam leo, Ijumaa, akikabiliwa na tuhuma za kutumia nafasi zake vibaya.
Kaimu huyo anakabiliwa na mashtaka mawili yanayohusishwa na utoaji wa leseni kwa makampuni ya Tanzanite One Mining Limited na State Mining Company. Hata hivyo,kaimu huyo aliyakana mashtaka yote mawili mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Victoria Nongwa.
Samanje ameachiwa kwa dhamana baada ya kudhaminiwa na watu wawili waliosaini bondi ya Shilingi milioni 50 kila mmoja. Mtuhumiwa huyo ametakiwa kutosafiri nje ya nchi bila kibali cha mahakama hiyo. Kesi hiyo imeahirishwa hadi Februari 28 kwa ajili ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza.
Post a Comment