Msanii wa miaka 21 Priscilla Opoku Kwarteng afariki dunia kwa ajali mbaya Ghana
Msanii kutoka nchini Ghana Priscilla Opoku Kwarteng maarufu kwa jina la Ebony Reigns, amefariki dunia katika ajali mbaya ya gari.
Ajali hiyo imetokea katika barabara ya Sunyani-Kumasi, Brong Ahafo. Kwa mujibu wa jeshi la polisi nchini humo limesema mrembo huyo (21) alikuwa kwenye gari aina ya Jeep 4×4, lenye namba za usajili AS 497—16.
Moja ya picha zilizopigwa kwenye ajali hiyo
Polisi hao wameongeza kuwa katika ajali hiyo watu wengine wawili waliokuwepo kwenye gari la msanii huyo ambao wanadaiwa ni wanajeshi wamefariki dunia walipofikishwa katika Hospital ya Mankranso.
Muimbaji huyo kwenye mtandao wake wa Instagram alikuwa anatumia jina la ebony_reigns na watu takribani 285k walikuwa wame-mfollow.
Post a Comment