Header Ads

Marekani kupitia ubalozi wake hapa nchini Tanzania imelaani mauaji ya Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasif, Daniel John


Marekani kupitia ubalozi wake hapa nchini Tanzania imelaani mauaji ya Katibu wa CHADEMA kata ya Hananasif, Daniel John na kuteswa kwa kada mwingine wa chama hicho, Reginald Mallya.
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe akiwaonyesha waandishi wa habari picha ya Kiongozi wa CHADEMA Kata ya Hananasif, Kinondoni, Daniel John.
Soma taarifa kamili iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania.
Marekani imesikitishwa sana na taarifa za kutekwa na utumiaji nguvu kikatili uliosababisha kifo cha Daniel John na majeraha kwa Reginald Mallya. Tunatuma salamu zetu za rambirambi kwa familia na marafiki wa marehemu kwa msiba huu. Kuongezeka kwa makabiliano ya kihasama na vitendo vya kikatili ni jambo linalotutia wasiwasi na kutusikitisha sana. Tunatoa wito kwa vyama vyote kulinda amani na usalama wa mchakato wa kidemokrasia, taifa na wa watu wa Tanzania. Aidha, tunaungana na Watanzania katika kutoa wito wa kufanyika kwa uchunguzi wenye uwazi ili kuwawajibisha wale wote wanaohusika na vitendo hivi vya kikatili kwa mujibu wa sheria za Tanzania.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali wasiliana na Ofisi ya Habari ya Ubalozi wa Marekani Dar es Salaam kwa simu namba: +255 22 229-4000 au kwa barua pepe:  DPO@state.gov.
 By  | 15 Febuari, 2018 | Categories: Tamko

No comments