Stand United KUPETA
Rekodi ya Mtibwa Sugar kutofungwa mechi zake za ugenini msimu huu katika ligi kuu bara ( Vodacom Premier League) imesitishwa kwa kukubali kipigo cha mabao 2-1 hapo jana dhidi ya Stand United, katika mchezo uliofanyika uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga.
Wana tam tam hao walikuwa wa kwanza kupata goli lake kupitia kwa kiungo mshambuliaji machachari, Salum Kihimbwa katika dakika ya 25 ya mchezo huo na hadi mapumziko ilikuwa ikiongoza.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi lakini na kuifanya timu ya Stand United kupata bao la kusawazisha dakika ya 79 kupitia kwa Bigirimana 79′ nakisha kuhitimisha karamu hiyo ya mabao kwa mchezaji, Tariq Seif 87′.
Namchezo huo wa Jumapili ya wiki hii kuifanya Mtibwa Sugar kuaribu rekodi yake ya kutokufungwa ugenini baada ya kucheza michezo 16 ya ligi kuu na kujikusanyia pointi 26 huku ikiendelea kushika nafasi ya tano katika msimamo.
Mabingwa wa ligi kuu bara mara mbili Mtibwa Sugar bado wanasalia Mkoani Shinyanga kwakuwa wanataraji kushuka tena dimbani siku ya Jumatano hii dhidi ya Mwadui katika mchezo utakao chezwa Mwadui Complex.
Post a Comment