Header Ads

Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amelaani vikali siasa za kujitenga

Image result for Waziri Mkuu wa India Narendra Modi


Waziri Mkuu wa India Narendra Modi amelaani vikali siasa za kujitenga ikiwa ni katika ishara ya onyo kwa mwenzake wa Canada, ambaye ziara yake ya wiki nzima nchini India imegubikwa na madai kuwa utawala wake hauwachukulii hatua watu wa itikadi kali wa madhehebu ya Sikh.

Akiwa amesimama kando ya Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau, ambaye yuko ziarani India, Modi alisema nchi yake haitawavumilia wale wanaotaka kuupinga uadilifu wake. 

Amesema hakuna nafasi ya watu wanaoitumia dini vibaya kwa ajii ya maslahi yao ya kisiasa na kueneza siasa za utengano. Ijapokuwa hakuwataja Masikhi kwa jina, maneno yake yalionekana kuashiria madai kutoka kwa baadhi ya watu wa jamii hiyo wanaotaka kuwa na jimbo lao kutoka kwa India.

No comments