alichomwa visu mara kadhaa baada ya kujaribu kumuokoa mwanamke
sipicha halisi ni kwa msaada wa mtandao
Mwanaume mmoja mwenye umri wa makamo chini Kenya katika eneo la Tudor Mombasa, ameuawa kwa kuchomwa na visu akijaribu kuwasuluhisha wapenzi waliokuwa wakigombana nyumbani kwao.
Kwa mujibu wa mjumbe wa nyumba 10 wa eneo hilo Benson Okello. Marehemu alichomwa visu mara kadhaa baada ya kujaribu kumuokoa mwanamke mmoja mwenye umri wa miaka 25 aliyekuwa akipigwa na mume wake, akimtuhumu kutumia dawa za kupanga uzazi ili asimzalie mtoto.
Okello amesema tukio hilo limewaacha pia wenza hao wakiwa wamejeruhiana vibaya na kupelekea kukimbizwa hospitali, ambako wamelazwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi.
Kwa mujibu wa majirani wamesema wawili hao wamekuwa watu wa kugombana mara kwa mara, kwa sababu hiyo hiyo ya kutumia njia za uzazi wa mpango.
Post a Comment