Header Ads

Pierre Emerick Aubameyang hakuwa na wakati mzuri katika uwanja wa nyumbani

B
Fußball Bundesliga | 20. Spieltag | Borussia Dortmund - SC Freiburg | Pierre-Emerick Aubameyang (picture-alliance/dpa/G. Kirchner)
 Lakini Pierre Emerick Aubameyang hakuwa na wakati mzuri katika uwanja wa nyumbani wa Signal Iduna Park. Alifurukuta uwanjani bila kufanya chochote na alizomewa na mashabiki wa timu yake.
Sasa ripoti za Ujerumanin na Uingereza zinasema kuwa uhamisho wake wa kwenda Arsenal unakaribia. Gazeti la Ujerumani la KICKER limeripoti kuwa Arsenal na Dortmund wamekubaliana bei ya euro milioni 63 kwa ajili ya uhamisho wa Mgabon huyo mwenye umri wa miaka 28…na kama sehemu ya makubaliano hayo, mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud huenda akahamia Ujerumani kwa mkopo hadi mwishoni mwa msimu. Lakini ripoti hiyo imesema Giroud bado anatafakari kuhusu mkataba huo maana angependelea kubakia England huku Chelsea ikionekana kumuwinda. 

No comments