Israel yashambulia Syria
Israel yashambulia Syria
imeshambulia kile ilichosema ni maeneo ya Iran ndani ya Syria Jumamosi (10.02.2018)katika shambulio kubwa baada ya moja kati ya ndege zake za kivita kushambuliwa na mfumo wa ulinzi wa nga wa Syria na kuanguka
Kufuatia makabiliano makubwa kabisa baina ya mahasimu hao wakubwa Israel na Iran tangu vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Syria kuanza mwaka 2011, waziri mkuu Benjamin Netanyahu aliapa kuizuwia Iran kuweka majeshi yake katika taifa hilo la Kiarabu.
Marekani imeiunga mkono Israel na kuilaumu Iran kwa kuchochea uhasama. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa wito wa "kuachana na hali ya kuchochea ghasia haraka na bila ya masharti" nchini Syria, msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephane Dujarric alisema katika taarifa.Mashambulizi ya Israel yamekuja baada ya kuingilia kati kile ilichosema kuwa ni ndege isiyokuwa na rubani ya Iran iliyoingia katika anga lake kutoka Syria, na kuiita kuwa ni "shambulio".
Ilikuwa mara ya kwanza Israel kukiri hadharani kwamba imelenga kile ilichokieleza kuwa ni maeneo ya Iran nchini Syria tangu mzozo huo kuanza. Iran imeshutumu kile ilichosema kuwa ni "uongo" wa Israel na kusema Syria ina haki ya kujilinda dhidi ya mashambulizi. Katika hali tofauti, Iran imetoa taarifa pamoja na washirika wakuu wengine wa Syria, Urusi na kundi la wanamgambo wa Lebanon la Hezbollah, wakikana madai ya ndege isiyokuwa na rubani yaliyotolewa na Israel.Uongo wa Israel
Msemaji wa jeshi la Israel Jonathn Conricus ameonya kwamba Syria na Iran "zinacheza na moto", lakini alisisitiza kwamba nchi yake haitaki kuendeleza mzozo huo. "Huu ni ukiukaji mkubwa kabisa wa mipaka ya Israel kufanywa na Iran" katika historia ya miaka ya hivi karibuni, Conricus aliwaambia waandishi habari.Wizara ya mambo ya kigeni ya Urusi imetaka kuwepo na "kujizuwia" kutoka pande zote, na kuongeza kwamba "haikubaliki kuanza kutengeneza mazingira ya vitisho kwa maisha na usalama ya wanajeshi wa Urusi" ndani ya Syria.
l
Israel ilisema kulipiza kisasi ilifanya "mashambulizi makubwa" dhidi ya mfumo wa ulinzi wa anga wa Syria na maeneo ya Iran. "maeneo kumi na mbili, ikiwa ni pamoja na vifaa vitatu vya ulinzi wa makombora ya angani pamoja na maeneo manne ambayo ni sehemu ya jeshi la Iran nchini syria vilishambuliwa," taarifa ya jeshi imesema. Marubani wawili waliokuwamo katika ndege chapa F16 wako hai baada ya kuruka kutoka katika ndege hiyo, licha ya kuwa walijeruhiwa vibaya, jeshi lilisema.
Post a Comment