Header Ads

Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa, Geofrey Nyang'oro amekamatwa na polisi.



Mwandishi wa gazeti la Mwananchi mkoani Iringa, Geofrey Nyang'oro amekamatwa na polisi.

Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoa wa Iringa (IPC), Frank Leonard ameiambia Malunde kuwa mwandishi huyo wa habari amekamatwa na polisi wakati akiwa katika mahakama ya wilaya ya Iringa leo Alhamis Februari 15,2018.

Amesema wanaendelea kufuatilia sababu za kukamatwa kwake na yupo chini ya ulinzi kwa mahojiano.


"Ni kweli tumepata taarifa za kuwa Nyang'oro amekamatwa kwa mahojiano na mkuu wa upelelezi wa makosa ya jinai (RCO) tunafuatilia kujua zaidi" amesema.

No comments