Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatofautiana kuhusu wazo la kuweka masharti mapya ya kupokea fedha
Viongozi wa Umoja wa Ulaya wanatofautiana kuhusu wazo la kuweka masharti mapya ya kupokea fedha za Umoja wa Ulaya, ikiwemo kuonyesha mshikamano kuhusu utoaji hifadhi kwa wakimbizi miongoni mwa wanachama. Hayo yamejitokeza wakati viongozi hao wakikutana leo mjini Brussels kwa ajili ya mazungumzo ya mwanzo kuhusu mipango ya muda mrefu ya bajeti ya Umoja wa Ulaya.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel aliwaambia wabunge kuwa vigezo vya kugawa fedha kutoka Umoja wa Ulaya katika siku za usoni vinapaswa kuonyesha nia ya maeneo mengi na serikali za mitaa katika upokeaji na ushirikiano wa wakimbizi.
Pendekezo lake limezusha hisia tofauti ambapo baadhi ya viongozi wa Ulaya wanasema lengo kuu la fedha za Umoja wa Ulaya ni kuzisaidia nchi masikini za umoja huo.
Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Jean-Claude Juncker ameonya kuwa hataki migawanyiko kuhusiana na bajeti isababishe mpasuko mkubwa kati ya mataifa wnaachama katika upande wa mashariki na magharibi mwa Ulaya.
Post a Comment