Header Ads

simba ya tamba


Image result for picha ya simba
EMMANUEL Okwi jana aliipatia Simba pointi muhimu baada ya kuifungia bao katika ushindi wa 1-0 dhidi ya Azam kwenye mechi ya Ligi Kuu iliyochezwa Uwanja wa Taifa.
Ushindi huo unaifanya Simba izidi kujikita kileleni kwa kujikusanyia pointi 41 juu ya Azam na mabingwa watetezi, Yanga wenye pointi 34 na Azam yenye pointi 33. Iliichukua Simba dakika 37 kuandika bao pekee katika mechi hiyo ambayo vinara hao wa ligi walitawala zaidi kipindi cha kwanza.
Okwi alifunga bao hilo baada ya kuunganisha krosi safi ya Asante Kwasi kabla ya kuujaza mpira wavuni. Kabla ya kufunga bao hilo, Okwi ‘Mhenga’ alipata nafasi kadhaa za kufunga katika dakika ya 5, 24 na 28 ambapo zote ama zilidakwa na kipa wa Azam Razak Abalora au zilitoka nje.
Azam ilionekana kubadilika katika kipindi cha pili ambapo benchi lake la ufundi lilianza kwa kufanya mabadiliko kwa kumtoa Mbaraka Yusuf na kumuingiza Shaaban Iddi. Mabadiliko hayo yaliifanya timu hiyo kubadilika kwani sasa mashambulizi yalifika langoni mwa Simba na dakika ya 49 Yahaya Zaud alipata nafasi lakini alipiga mpira pembeni.
Aidha katika mechi hiyo kulikuwa na ubabe wa hapa na pale ikiwa ni pamoja na mfungaji wa bao la Simba Okwi kufanyiwa madhambi ya mara kwa mara na mabeki wa Azam. Pengine hiyo ndio sababu ya benchi la ufundi la Simba kumtoa nyota huyo wa Uganda katika dakika ya 84 na nafasi yake kuchukuliwa na Nicholas Gyan.
Katika mechi nyingine za ligi zilizochezwa jana, Mwadui imeutumia vema uwanja wake wa nyumbani kwa kuichapa Mtibwa Sugar mabao 3-1 huku Mbao ikishindwa kufanya hivyo kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-1.
Simba: Aishi Manula, Shomary Kapombe, Erasto Nyoni, Yussuph Mlipili, Asante Kwasi, Jonas Mkude, Shiza Kichuya, Said Ndemla/ Muzamil Yassin dk59, John Bocco, Emmanuel Okwi/ Nicholaus Gyan dk84, James Kotei.
Azam FC:Razak Abalora, Daniel Amoah, Bruce Kangwa, Yakubu Mohammed, Aggrey Morris, Stephan Kingue, Iddi Kipagwile/ Salum Abubakar dk55, Frank Domayo, Mbaraka Yussuph, Yahya Zayed/Bernard Arthur dk71,Enock Atta-Agyei

No comments