Ajiua kisa wivu kwa mke wake
Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 43, Nicholas Wambua anayeishi katika eneo la
Pipe Line Mjini Nairobi nchini Kenya, amejiua kwa kunywa sumu baada ya kumuhisi mkewe
akimsaliti.
Mwanaume huyo ambaye alikuwa akifanya biashara ya mitumba katika eneo hilo, amefanya
tukio hilo asubuhi ya Jumapili hii huku akiaacha ujumbe kwa watu wake wa karibu wamwambie
mke wake huyo awaangalie watoto.
“Aliniambia ankwenda mbali na kuniomba nimwambie mama Sharon awaangalie watoto wake
kwa ajili yake, ahtukujua akimaanisha kifo”, amesema Bi. Tabitha Bernad ambaye ni mkwe wa marehemu Wambua.
Mkwe wake huyo ameendelea kwa kusema kwamba mara nyingi marehemu alikuwa
akimlalamikia kuwa mke wake ana tabia ya kuleta wanaume tofauti tofauti nyumbani kwao
na kulala nao, iliniumiza kwa kweli lakini hatukupata muda wakuzungumza zaidi”, amesema
Bi. Tabitha ambaye pia ni mkwe wa marehemu.
Post a Comment