Sifa za Mwanamke wa Kuoa
Mithali 14:1“Kila mwanamke aliye na Hekima hujenga nyumba yake; Bali aliye mpumbavu hibomoa kwa mikono yake mwenyewe”
Kuna mithali isemayo “MAJUTO MJUKUU”, ni kawaida kwa wanandoa kuangalia na kulaumiana juu ya matatizo yanayojitokeza, badala ya kutafakari chanzo cha matatizo. Matatizo mengi ya ndoa yanatokana na wanandoa kutokuwa na elimu ya ndoa na kutofuata ushauri wa Mungu aliyeanzisha Ndoa. Baadhi ya sifa za Mwanamke mwenye Hekima – Pia Soma Mithali 31:10-31.
1. Hufumbua kinywa chake kwa hekima, Na sheria ya wema I katika ulimi wake (31:26). Wanawake wengi hawajui kuutumia ulimi vizuri – Ukali, maneno ya mikato, matusi, ukaidi n.k. kwao ni mambo ya kawaida. Wengi wanatawaliwa na HASIRA na WIVU, akiona mumewe anacheka na mwanamke ni Kosa la jinai, mwanamke anafura wala hata hawezi kuongea, hali ya hewa inabadilika hata paka nyumbani wanatambua kuwa hali ni Mbaya.
2. Hufanya kazi kwa Moyo na Huamka alfajiri na mapema
Kuna wanawake ambao ni wavivu kupindukia, inafika wakati hata kutandika kitanda anamtuma House Girl, wanaume ni rahisi sana kuvutwa na anayemhudumia kwa ukaribu, House girl akiandaa chakula, mara kitanda, mara maji ya kuoga, mara apige deki chumbani n.k. Haichelewi mwanaume kulipa fadhila kwa wema anaotendewa.
3. Ni msafi na anajua kuandaa mavazi yanayofaa kwa familia yake
Kuna wanawake ambao ni wachafu – usishangae kukuta sufuria kwenye makochi, chumba cha kulala ni stoo ya nepi za mikojo na nguo chafu, wengine kuoga ni anasa. Mwanamke ni MAJI, sharti mwanamke awe msafi muda wote. Wanaume wote wanapenda Usafi, marashi hata ya mchina yasikose, Mwanamke hakikisha “Reception” inakuwa Safi na kuwa katika hali ya kumfanya Mume ajisikie kujipumzisha kwa Raha mstarehe.
4. Jali na timiza Mahitaji ya NDOA kwa mume wako
Sulemani anasema mwanamke mwema “Taa yake haizimiki usiku”, kuna wanawake wavivu kwa swala hili, pia kuna wanaopenda kulipa visasi kwa kuwanyima waume zao huduma, utakuta wiki nzima mama apanda kitandani huku amevaa “KOMBATI” utafikiri ni askari anaenda vitani. Wanaume ni sawa na Mbuzi ambao hawachelewi kukata kamba wakikosa majani walipofungiwa. Fanya makosa yote, lakini usijefanya ujinga wa kumkomoa mume kwa kumnyima huduma ya Ndoa, hilo ni kosa la Jinai. Hakikisha huduma hizo zinaboreshwa, nenda na wakati ili mradi isiwe kinyume na taratibu za Mungu.
5. Mwanamke anatakiwa kujua kupika chakula kitamu, ambacho familia itafurahia.
Wanawake wengi hasa wa siku hizi hawajui kupika, ndio maana utakuta wanaume wengi wanaishia kula hotelini au kwa mama ntilie, kama umetoka bara basi usione aibu kujifunza kwa watu wa pwani namna ya kuunga NAZI kwenye chakula. Akina mama ni wajibu wao kujifunza Mapishi, Mchicha peke yake unaweza kuwa na mapishi zaidi ya 10, wanaume wanapenda chakula chenye ladha “Test”, mfanye mume akumbuke chakula cha nyumbani.
6. Mwamini Mume wako,
wivu na hisia mbaya ni adui wa ndoa yako. Usitoe siri za ndoa yenu kwa mashoga au ndugu zako. Muda wote muombe Mungu akupatie hekima ya kuongea pindi tatizo linapotokea, Muombee mume wako ili Mungu amsaidie pia awe na Hekima ya kutunza Ndoa kwa Uadilifu na Upendo.
kali blog
Sifa za Mwanamke wa Kuoa
Wanaume wengi wanapofikia hatua ya kuoa si kwamba wanakurupuka tu na kuoa mwanamke yeyote mwenye sura nzuri, bali huchukua muda wao mwingi kuchunguza mambo mengi juu ya wake ambao wanadhani kwamba wanaweza kuwa pamoja kwa kipindi chote cha maisha.
Wanawake wengi wanajisahau na kudhani kwamba kitu kinachowezakuwafanya wakapata wachumba niuzuri hivyo kupoteza muda wao kujichubua na kujiremba ili wawavutie wanaume bila kujua kwamba kuolewa ni zaidi ya uzuri.
Hali sasa hivi imebadilika ni tofauti na kipindi cha nyuma ambapo ukiwa na sura nzuri na umbo la kuvutia basi una asilimia 100 za kuolewa.
Utafiti ambao nimeufanya unaonesha kwamba zaidi ya uzuri wa tabia na umbo, kuna kuna sifa nyingine za msingi ambazo mwanamke anatakiwa kuwa nazo ili aweze kuwa katika mazingira mazuri ya kupata mchumba wa kumuoa kiasi kwamba asipokuwa nazo ataishia kuchezewa tu lakini haitatokea mtu kumtakiwa kwamba anataka kumuoa.
1. MWEYE MAPENZI YA KWELI
Lengo kubwa la mwanaume kuoa ni kutaka kupata mapenzi ya kweli kutoka kwa mwanamke na ikiwezekana waweze kupata watotoa ambapo watoto mara ndio wamekuwa furaha ya ndoa. Wapo wanawake wengine ambao wanonesha wazi kutokuwa na mapenzi ya kweli bali wanakuwa na mapenzi ya kuzuga. Wanachotaka wao aidha kupata umaarufu tu kwamba yuko na mtu fulani ama kuweza kupata pesa alizonazo mwanaume lakini sio kwamba ana mapenzi ya dhati kutoka moyoni mwake.
Mwanamke asiye na mapenzi ya dhati utamgundua tu, muda mwingiutamuona macho yake yako kwenye mfuko wa mwanaume. Akiona kwamba mfuko umetuna utaona anaonesha mapenzi ya hali ya juu lakini pindi hali inapokuwa kubwa mbaya kifedha mapenzi yanaanza kufifia.
Kwanini wanaume wanapenda wana wake wenye mapenzi ya dhati kutoka mioyoni mwao na si kutokana na fedha walizonazo? Hii inatokana na ukweli kwamba maisha siku zote yanabadilika, kama waswahili wanavyosema, kuna kupanda na kushuka.
Sio kwamba kila siku utakuwa na maisha mazuri na kama itatokea hivyo basi ushukuru mungu.Hivyo basi mwanamke wa kuoa lazima afahamu hivyo na awe tayari kuonesha mapenzi yake ya dhati wakati wote wa maisha yao na si kwa kipindi fulani tu cha neema.
Si hivyo tu pia asilimia kubwa ya maisha ya ndoa yanatawaliwa na mapenzi, kwa hiyo nyanja hiyo inakuwa ya msingi sana kwa wanaume wengi kuiangalia ili wasije wakajikuta wanaoa mwanamke ambaye baada ya muda mapenzi yanakwenda likizo hali ambayo inaweza kuwafanya wasiishi maisha ya raha mustarehe.
2. WENYE TABIA NZURI
Tabia njema ndio silaha ya maisha, ukiwa na tabia nzuri kila mtu atakupenda, hiyo ni katika maisha ya kawaida. Lakini linapokuja sualana kuoa tabia inakuwa kitu cha awali sana kungaliwa na hiyo inaweza kuwa na ukweli kwa sababu wapo wasichana wazuri wenye mvuto wa aina yake na maumbile mazuri, lakini wanakosa wanaume wa kuwaoa, ukiuliza kwani utaambiwa anatabia mbaya.
Naweza kusema hilo ndilo limekuwa tatizo kubwa kwa baadhi ya wanawake kukosa wanaume wa kuwaona. Hakuna mwanaume hata mmoja kati ya wale ambao nimejaribu kuongea naye ambaye ameonesha kulidharau suala hilo la tabia.
Si hivyo tu wapo wanaume ambao wameingia kichwa kichwa na kuoa kwa kuangalia sura tu bila kujali tabia, matokeo yake baada ya siku chache yanatokea machafuko ya aina yake hali ambayo imepelekea kuvunjika kwa ndoa kutokana na tabia mbaya alizonazo mwanamke.
3. WENYE UCHU NA MAENDELEO
Hivi karibuni kumekuwepo na mabadiliko ya aina yake kwa wanaume, wengi sasa hivi hawapendi kabisa kuoa mwanamke ambaye hana kazi yaani 'golikipa'. Kama atakuwa hana kazi basi awe na uchu wa maendeleo kwa kujituma kufanya kazi mbalimbali za kimaendeleo kama vile kilimo kwa wale walio vijijini na biashara ndogondogo kwa wale ambao wako mijijini na hata vijijini.
Ile dhana ya kusema mwanamke ni mama wa nyumbani wa kukaa na kujipodoa akimsubiria mwnaume arudi amstarehesha, sasa hivi imepitwa na wakati. Wanaume wengi wanapenda wanawake ambao ni wahangaikaji, wenye ndoto za maendeleo katika maisha yao. Hata kama watakuwa si wafanyakazi lakini wawe wenye kutoa ushauri kwa waume zao juu ya jinsi gani wafanye ili wafanikiwe.
4. WASIOPENDA MAKUU
Kuna wanawake wengine wanakuwa na tabia za ajabu sana kiasi kwamba yaweza kuwa kero kwa wanaume. Wapo wanawake ambao wanapenda makuu bila kujali hali halisi ilivyo. Kuna wanawake naweza kusema wana tamaa, kila wikiendi utamsikia "leo tunakwenda wapi dear?"
Akimuona rafiki yake kanunua simuya laki tatu na yeye utamsikia akisema, ‘na mimi naomba uninunulie simu kama ya Grace’. Ukienda naye Pub anakuambia,"mimi sinywi pombe za chupa natumia za kopo tena Heineken’. Yeye hajali kiasi cha pesa mwanaume alicho nacho na usipotekelezea anachukia na anaweza hata kupunguza mapenzi.
Wanawake kama hawa wako katika mazingira magumu sana ya kuweza kupata wanaume wa kuwaoa. Mara nyingi katika maisha fedha huzungumza, kama mwanaume atakuwa na pesa ya kutosha itakuwa rahisi sana kwa mwanamke kupata kila atakachopenda lakini si kwa kumwambia mimi nataka kitu fulani.Mwanaune mwenyewe utamsikia akisema, ‘unataka nikununulie simu ya aina gani, au leo unataka twende wapi?’ hapo ndipo utakuwa na nafasi ya kusema, ‘mimi nataka uninunulie simu kama ya fulani ama leo nataka twende sehemu fulani.’
Wanaume ni warahisi sana wa kuwapatia wale ambao wanatarajia kuwaoa chochote ambacho watahitaji kama tu pesa haitakuwa tatizo. Kitu ambacho kinawaudhi wanaume wengi ni ile tabia ya mwanamke kupenda mambo makubwa bila kuangalia uwezo uliopo kwa mwanume.
Kuna wanawake wengine wao si wasemaji kabisa, yeye anasubiri leoamemletea hiki, anapokea na kushukuru, kesho akiambiwa twende beach anakubali. Au wengine wanasubiri mpaka waulizwe wanataka nini, ndio wanasema.
Sisemi kwamba uwe mkimya tu hata kama una shida ya kitu fulani na unafahamu kwamba ukimweleza mwenza wako anaweza kukusaidia, hapana! kama unaona kwamba uwezekano wa kupata kile ambacho unakihitajiupo mweleze kwa utaratibu naamini atakuelewa na kukutimizia.Tabia ambayo hawaipendi wanaume wengi ni ile ya kulazimisha ufanyiwe kitu fulaniwakati inawezekana uwezekano haupo.
5. WAVUMILIVU
Wapo wanawake ambao sio wavumilivu kabisa katika maisha.Tunajua kwamba maisha siku zote hayatabiriki, yanaweza kutokea matatizo ya kiafya ama kifedha.Huu ndio wakati wa kuona uvumilivu wa mtu.Kama mwanamke anatarajia kwamba siku zote ni za raha tu na pindi matatizo yanapotokea anachukua uamuzi wa kumtoroka mwanume, huyo siyo mwanamke wa kuoa.
Wangapi leo hii huwatoroka waume zao pindi inapotokea kuumwa, kufilisika ama kupatwa na tatizo lolote ambalo kwa namna moja ama nyingine yanaweza kuwafanya maisha yao kutingishika?
Uvumilivu kwa mwanamke utakuwepo kama tu atakuwa na mapenzi ya dhati kama nilivyozungumza hapo awali. Mwanamke mweye mapenzi ya dhati ni lazima atakuwa mvumilivu na atakuwa tayari kuishi katika maisha ya aina yoyote, yawe ya raha ama ya starehe.Hawa ndio wale ambao wanaume wengi wengependa kuwa nao maishani mwao.
Licha ya kupenda kuoa wanawake amabo wana tabia hizo nilizozitaja hapo juu, wanachukizwa sana na wanawake ambao wanavijitabia vidogo vidogo ambavyo kimsingi havikubaliki katka jamii.
Tabia hizo ni kama wambea, wasio wakweli na wawazi, wasioridhika, wagumu kusamehe na wapesi wa kuchukia, wagomvi na wenye roho ya kwanini.
Utafiti huu umefanyikwa kwa baadhi ya wanaume ambao wanatarajia kuoa wanawake ambao wanaoishi katika maeneo mbalimbali
Kwa maana hiyo basi hiyo iwe changamoto kwa wanawake. Wajue kwamba wanaume wanafurahi kuwa na wanawake wa aina gani. Hata kama utakuwa umeshaolewa, kama kuna wakati kunakuwa na kutokuelewana baina yenu, chunguza yawezekana kwamba unakosa mojawapo ya tabia ambazo nimezitaja hapo juu. Waweza kubadilika kwani inawezekana.
AINA ZA WANAWAKE AMBAO WANAUME WANAPENDA
Sometimes Wanawake huwa wanajiuliza Maswali mengi,wafanyeje ili wapendwe,wanahisi wana bahati mbaya,kila wanapojitoa mioyo yao inaumizwa.Jamaa hawakai,wanatupia kitu,wanakula mzigo wanatembea na Bwana..Mioyo yao imejaa matundu na hawaamini kabisa kama Wanaume huwa wanapenda,imefikia point wanadhani Wanaume hutamani tu kumbe SI KWELI!
Wanaume nao wana taste zao,hawaendi tu kama Mbwa koko,jalala moja baada ya jingine,HAPANA…Know their taste and you will enjoy theirs.
Sifa za Mwanamke ambae Mwanaume atavutiwa na kukaa ni hizi zifuatazo,JITAZAME,kama huna any of these,you better try to learn to have them,its not too late:
1.MWANAMKE MWENYE MSIMAMO
Jambo moja muhimu,the number 1 thing ambacho Mwanaume anaangalia kwa Mwanamke ni Msimamo wako…Sio Mwanamke uko kama Feni,kila sehemu unapulizia upepo,Mashariki,Magharibi kote wewe…Hapo sahau,tena sahau sana.Mwanaume anahitaji kuwa na uhakika,Mwanamke aliyemkabidhi moyo hana mishemishe na hayumbishwi na lolote,na chochote na penzi lake liko safe
Unaweza kuwa na kila kitu,Mzuri wa Sura na kila kituuuu,na bado usimpate Mwanaume wa Maana kama huna sifa hii,hakuna muujiza kwenye hili,ndo wanaume walivyoumbwa,if you lack this hamna Mwanaume wa Maana utapata,utapata vimeo kama ulivyo!
2.MWANAMKE MUELEWA
Men are simple creatures,they love to live simple,and take them simple as they are…
Ukiwa aina ya Mwanamke unamind vitu…kitu kidogo ugomvi…Unaongea na nani…Uko wapi..Na nani,Kwanini,hee,jamanikama Mahaakama kuu??Hapa unapoteza Credits
Kuwa aina ya Mwanamke muelewa ambae utamfanya Mwanaume ajisikie vibaya kufanya kitu flani ambacho ulishamwambia asifanye before…Lakini sio kukaripia na kununa kwa sababu amerudia..let him realize that amefanya kitu cha kukuudhi na hujareact,and if hes aman enough,he will know and apologize
Ila kama ni gumegume basi tena,litakausha na ndo inakuwa issue hapo…Are u patient enough to handle it??kazi kwako,ila kuna wanawake wana uwezo huu,learn from them wamewezaje..No matter how complicated the man is,they know how to handle him
Jua Lugha ya kutumia ambayo utafikisha ujumbe and yet you dont show him kwamba umemind na unamkaripia…kumkaripia Mwanaume ni msala mpya,hata kama ana kosa atakumind na itakula kwako…Una ulimi mzuri kufikisha ujumbe??
3.MWANAMKE DIRECTOR
Baba ni kichwa cha nyumba….mimi huamini Mama ni macho yaliyo kwenye kichwa hicho
Women play a very vital role in DIRECTING THE HEAD TO THE RIGHT WAY
Kichwa bila macho si utajigonga tu????Mwanamke ni jicho…
Ukikalia kujiremba tu na kuwaza mambo mengine bila kujua kuna kichwa kinasubiri maelekezo yako,utaonekana bogus..kutwa uko kwenye Umbea,huna muda wa kujua ur man anafanya nini,ana plan gani mwaka huo,unamsaidiaje kuzifikia,sasa we faida yako nini kwenye maisha yake??
be the kind of a woman ambae Mwanaume aki-achieve jambo anasema I have a woman beside of me who engineered this…Kama hujawahi kufikia hatua ya kuwaappreciated na ur man kwa jambo hili jua kuna mahali umefeli…Na hili haliji hivihivi,linakuja pale kunapokuwa na proper communication between you and ur man…Bila good communication:
1.Hutajua what ur man is up to
2.Kwa sababu hujui what he is up to hutakuwa na msaada.
3.Akifaulu,jua haupo kwenye picha ya mafanikio yake na ur simply useless
4.Akifeli,ur part of his failure kwamba humsaidii lolote..ur simply useless and actually absent in his life kwa sababu uwepo wako haumsaidii its better he becomes alone!YOU HEARD???
Women have planning and control ability,USE IT…Usikae tu kama muuza genge unasubiri wateja,Do your job and Win him!
4.MWANAMKE MSAFI NA MZURI
Usafi huu sio wa nguo tu na kunukia,ni zaidi ya hilo…
Usafi unaanzia ndani..Msaidie Mwanaume awe msafi pia,rohoni hadi mwilini…Rohoni how???Jitu halisali,halikumbuki kuna Mungu,lipo tu,unadhani mtajenga Familia gani baadae???
Msaidie kum-remind kukumbuka hilo,Mafanikio ya nje huanzia ndani..Dirty inside,Dirty Outside…Mambo mengine anafanya nje na yanaku-affect kwa sababu umefeli ku-inspire change ya ndani…Ngumu hii lakini ndo hivyo..You cansave a lot of energy kama atakuwa msafi wa ndani,everything outside will be set automatically…Whatever u see in physical started in Spiritual…Yeah right! Hata ulimwengu uliumbwa,na vyote unavyoviona baada ya Plan ya Spirit kumalizaika.Soma Kitabu cha Mwanzo kwenye Biblia,uone Uumbaji ulifanyikaje…Same applies na hapa,Uumbajiwa vitu vya nje,Mahusiano imara,Familia bora,inajengwa ndani..
Sio kazi yako ni kuuliza Baby hatuendi Club,Baby this…Unamkumbusha kusali???Utatengeneza mme freemason bila kujua…Mtu hasali we upo tu unaona sawa…CHANGE!
Huu usafi mwingine wanawake mmejaliwa,biashara za kunuka kikwapa no,Kusafisha nyumba vema saafiii…mengine si kama kawa??Mpango mzima uko hapo.
Uzuri huwa ni subjective…Unaweza kuwa mzuri kwangu lakini ni wa kawaida kabisa kwa mwingine….Ukiwa msafi unaweza ukamfanya Man wako aone potential,hata kama wewe sio mzuri sana lakini anaona Kiongozi wa Familia inside you and he will definitely opt you.
SIFA MUHIMU ZA KUZINGATIA UTAFUTAPO MTU WA KUISHI NAYE;
MARA nyingi vijana hupata taabu sana katika suala la kuchagua mchumba. Vijana wa kiume ndio hasa hupata wakati mgumu zaidi kwani jamii imewapa wajibu wa kuanzisha mazungumzo yahusianayo na mapenzi. Hata hivyo,vijana wa kike nao wanao wajibu wa kuchagua ili kuhakikisha kuwa hawaanguki mikononi mwa mabazazi wa kuwalaghai na kuwatumia kwa raha za miili yao kisha kuwaacha kwenye mataa.
Ni jambo la kawaida kwa vijana walio wengi, wawe wa kike au wa kiume, kuangalia sura na mwonekano wa mtu. Lakini unapotafuta mchum ba kwa malengo ya kuishi naye maisha yakoyote kama mume na mke haipendezi kuangalia tu mwonekano, maana Waswahili husema si kila king’aacho ni almasi. Kwa sababu hiyo, hapa yatabainishwa mambo muhimu ya kuangalia na kuzingatia katika suala hili.
1.UADILIFU
Pamoja na sifa zote za uzuri zinazoweza kubainishwa na kufanywa kuwa vigezo vya uzuri wamwanamke na mwanaume na hata zikatumiwa kumpata Miss au Mr Tanzania, sifa kuu impasayo mtu anayefaa kuwa mchumba kuwa nayo ni sifa ya uadilifu.
Mtu anapokuwa na uadilifu (pengine uaminifu), maana yake ni kwamba tabia ya mtu huyu anayoionesha nje ndiyo tabia yake halisi na anapofanya jambo jema analifanya kwa roho yake na si kwa unafiki.
Mtu anapokuwa mwadilifu ataheshimu maadili na kufanya wema, hata pale inapokuwa rahisi kwa wengine kukengeuka na kufuata njia za mkato ambazo mara nyingi si za halali.
Mtu mwadilifu pia huwa na sifa za ukweli na kujitolea kuwasaidia watu wengine bila kujali faida – haya yote ni mambo muhimu ambayo mtu mwenye kuwa nayo huwa na msingi wa ujenzi wa uhusiano imara na wa kudumu.
Watu wanaoweza kujivunia furaha ya kweli katika maisha yao ya ndoa, ni watu ambao wamekutana wote wakiwa na sifa ya uadilifu ambayo hujumuisha mambo mengi.
Zipo ndoa nyingi zenye furaha ya bandia. Furaha hii mara nyingi hutokana na ridhiko la kimwili alipatalo mtu kutokana na kukidhiwa kwa mahitaji yake ya kimwili yanayohusiana na haki za msingi za binadamu – yaani chakula,mavazi na malazi. Lakini furaha ya kweli ya maisha ya ndoa, watu hawaipati isipokuwa katika uhusiano ambao wenza wamethibitishana kuwa waadilifu.
2.HEKIMA
Mtu mwenye uadilifu wa kweli, mbali na kuwa mwema kwa mwenzake, pia huhakikisha anakabiliana kwa busara na hekimana matatizo yote yanayoweza kusababisha kuyumba kwa uhusiano, hususan yale yaliyo nje ya uwezo wake.
Uzoefu unaonesha kuwa wapenzi, hususan wanandoa walio katika uhusiano wa muda mrefu wanaoendelea kufurahia unyumba wao si wale ambao walipendana kwa mvuto na wala hawana mambomengi ya asili yanayowaunganisha kuliko wale wanaotengana. Lakini la muhimu ni kwamba watu hawa huwa wamejifunza jinsi ya kukabiliana kwa hekima na matatizo yanayojitokeza, hususan yale yanayotokana na tofauti zao kimtazamo.
Ukiachilia mbali sifa ya uadilifu, watu hawa huwa wamejifunza kukabiliana na matatizo kuhusiana na uzazi na ulezi wa watoto, uhusiano na ndugu, jamaa na marafiki, suala la ngono, fedha na maisha ya unyumba kwa ujumla.
Habari njema ni kwamba uadilifu na hekima ni mambo ambayo mtu yeyote anaweza kujifunza na kisha kufanyia kazi. Ndiyo maana wanandoa hufundishwa kabla ya ndoa na hata wanapokuwa tayari wameoana huendelea kuhudhuria semina za kidini na kijamii kwa ajili ya kujiimarisha.
Kwa hiyo, kama mume/mke wako mtarajiwa anaonekana kuwa na utayari wa kujifunza kuhusiana na jinsi ya kuishi na mtu wa jinsia nyingine, ana nafasi kubwa ya kuwamke/mume mzuri baadaye.
3.UPOLE
Mfalme Suleiman katika mojawapo ya semi zake za hekima alisema mwanamke -- huibomoa nyumba yake kwa mikono yake. Yamkini ndivyo ilivyo pia kwa mwanaume --, maana upumbavu haujengi.
Siku zote kitu kinachovunja uhusiano wa kindoa si makombora ya nyuklia, bali ni ulimi. Kwa kadri mtu anavyoutumia ulimi wake anaweza kuijenga au kuibomoa nyumba yake.
Katika kumwangalia mtu ambaye unaweza kujenga naye nyumba ya kudumu, ni vema kumchunguza na kuhakikisha kuwa si mtu mwenye kupenda kurefusha maneno, maana hakika huyu atasababisha ugomvi mara kwa mara na uhusiano hautadumu.
Wapo watu ambao ndoa zao zina sifa ya ugomvi na karibu kila mtu anafahamu na hata wamekuwa kero kwa ndugu, jamaa na majirani zao, mara kwa mara wakiwaamsha watu usiku wa manane wakitafuta suluhu.
Mara nyingi wanaume ndio huanzisha ugomvi, lakini ugomvi huwa na nguvu zaidi kama mwanamke ni msemaji. Dawa ya kuzuia ugomvi usiokuwa na mpangoni kupunguza maneno na kuepuka kutafuta ushindi katika ubishi. Lakinikinga ya tatizo hili ni kuepuka kujiingiza katika uhusiano na mtu ambaye umejihakikishia kuwa si mwingi wa maneno.
Bahati nzuri, jamii huwatambua wanawake/wanaume ambao wanaweza kuwa wake/waume bora baadaye kwa hiyo ni wajibu wamtafutaji kuhakikisha kuwa anafanya uchunguzi wa kina kabla ya kujitosa kwa mtu ambaye baadaye atamtaabisha.
Mwanandoa aliyeifahamu vema dhana ya ndoa – kwamba ni maisha ya kuvumiliana na kuchukuliana, hufahamu ni wakati gani wa kusema na wakati gani wa kukaa kimya. Mtu huyu pia hufahamu njia nzuri na salama ya kujiondoa kwenye tatizo anapoona mwenzakeanaelekea kubaya, ili hatimaye uhusiano wao uendelee kuwa salama japo wao wanaweza kuwa wamekwaruzana.
Mtu huyu mwenye upole hujiweka katika mkao wa upatanishi na huhakikisha kuwa kila mjadala mkali unapita na kumalizika salama.Ni wazi kuwa katika kutafuta, kama hukukurupuka, utamwona mtu mwenye hulka hii – upole.
4.MVUTO
Hisia za mvuto wa kimapenzi ni muhimu katika kujenga uhusiano. Mtu mmoja akauliza, ni yupi bora – yule anayenivutia sana au yule anayenipenda sana? Maisha ni ya ajabu sana. Huwa inatokea kuwa mtu unayevutiwa naye sana yeye havutiwi nawe, bali anavutiwa na mwingine ambaye naye hana mpango naye!
Haya ndiyo maisha. Uzoefu unaonesha kuwa asilimia kubwa ya watu walio katika ndoa hawajawaoa/kuolewa na watu waliokuwa wakiwapenda sana enzi za ujana wao, au wale waliotimiza ndoto za ujana wao. Bahati njema miongoni mwa wanandoa hawa wapo wale wenye ndoa imara sana.
Mvuto wa kimapenzi ni muhimu sana, lakini watu husema maji yakisema usininywe yajibu kuwa wewe pia huna kiu nayo. Japo inaweza kuonekana kama ni aina ya‘sizitaki mbichi hizi’ lakini si vema kujisumbua na mtu asiyekupenda.
Badala ya kujihangaisha na mtu asiyekupenda, kaa chini na umsubiri anayekupenda hata kama huhisi kuvutiwa naye sana. Baadaye utamzoea na maisha yatakuwa mazuri, kisha utajiuliza baadaye yule aliyekuringia alikuwa na nini cha ziada?
Lakini iwapo mambo mengine yote yatakwenda sawa, ni vema na muhimu kabisa kuhakikisha kuwa mtu unayepanga kuwa naye maisha yako yote ni mtu anayekuvutia kimwili na kiakili, maana vinginevyounaweza kupata sababu ya kukidhi kiu yako nje – jambo ambalo si maadili mema katika ndoa na maisha.
NI MUHIMU KUWA MAKINI
Katika nyakati za ujana, watu wengihubabaishwa kwa mengi. Vijana wa kiume hubabaishwa na sura, maumbile na pengine rangi na kusahau mambo muhimu yaundayo orodha ya sifa za mke mwema.
Kwa upande wao, vijana wa kile pia waweza kubabaishwa na pesa, maumbile, sura, utanashati, umaarufu au kuchoshwa na shinikizo la umri, hivyo kujikuta wakijitumbukiza kwa wanaume wasio na sifa za waume wazuri.
Lakini tukirejea kwenye msemo wa zamani kuwa uzuri si hoja bora tabia, ni wazi kuwa tutafikia mahali tutajenga mahusiano imara na yasiyotikiswa na sunami zozote za kimaisha. Ilimradi tu uhakikishe kuwa mtu mwenyewe anakupa mvuto kimapenzi, maana vinginevyo kutakuwa hakuna maana.
Post a Comment