Header Ads

Image result for mlipuko wa bomu ngara


Wimbi jipya la mashambulizi ya mabomu limepiga mashariki mwa Ghouta nchini Syria kwa siku ya sita mfululizo, kabla ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kupiga kura ya kutaka mapigano yasitishwe kwa siku 30 kote nchini humo. 

Ndege za kivita zililishambulia eneo la kilimo lenye wakaazi wengi mashariki mwa mji mkuu, ikiwa ni ngome ya mwisho ya waasi karibu na Damascus. 

Mashambulizi hayo ya karibuni yamewaua watu 426 wakiwemo watoto 98.

 Mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Syria Staffan de Mistura ameomba pande zote kuweka chini silaha na kukomesha mashambulizi hayo ya kinyama ambayo ni mojawapo ya mabaya zaidi kuwahi kufanywa katika vita hivyo vya miaka saba. 

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatafakari kuhusu azimio, ambalo Kuwait na Sweden ziliandika, likitaka kusitishwa kwa mashambulizi kote Syria kwa ajili ya operesheni zote za kijeshi kwa siku 30 ili kuruhusu upelekaji wa misaada ya kiutu na kuhamishwa watu wanaohitaji matibabu.

Kura hiyo itapigwa baadaye leo.









chanzo dw

No comments