Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa yuro milioni 50 kwa jeshi la pamoja la kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel la Afrika Magharibi.
Umoja wa Ulaya umeahidi kutoa yuro milioni 50 kwa jeshi la pamoja la kupambana na ugaidi katika eneo la Sahel la Afrika Magharibi.
Akizungumza leo katika mkutano wa viongozi wa Ulaya mjini Brussels, Rais wa Halmashauri Kuu ya UIaya Jean-Claude Juncker alisema fedha hizo za ziada zitasaidia katika masuala ya utendaji wa jeshi hilo.
Ametoa wito kwa karibu viongozi 30 wa Umoja wa Ulaya na wa Afrika wanaokutana mjini Brussels, kuunga mkono juhudi za Burkina Faso, Chad, Mali, Mauritania na Niger kwa kutoa mchango katika kiwango kinachostahili ili kuifanikisha operesheni ya jeshi hilo la pamoja. Kikosi hicho
kinachofahamika kama G5 Sahel chenye askari 5,000 kinatafuta karibu yuro milioni 400 kwa ajili ya operesheni yake kwenye maeneo hasa ya mipakani, ikiwa ni pamoja na karibu na Libya - eneo linalotumiwa sana na wahamiaji wa Kiafrika kufunga safari za kuingia Italia.
Post a Comment